MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 13 August 2014

MAONYESHO YA SIKU YA WAKULIMA (NANE NANE) KANDA YA ZIWA YAFUNGULIWA RASMI JIJINI MWANZA.

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa sherehe ya siku ya maonyesho ya wakulima (nanenane) Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi Magalula akitembelea mabanda mbalimbali ili kujionea shughuli zinazofanywa na wakulima,wataalamu pamoja na wadau.

Mhe.Magalula Saidi Magalula Mkuu wa Mkoa wa Geita wakwanza kulia na Mhe. Evarist Ndikilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza wapili kutoka kulia  na viongozi mbalimbali wa Mikoa na Wilaya wakitembelea mabanda kujionea shughuli na bidhaa mbalimbali za kilimo wakati wa sherehe ya uzinduzi wa siku ya wakulima (nanenane)kanda ya ziwa.






Sunday 10 August 2014

Mgeni rasmi wa ufunguzi wa sherehe za maonyesho ya siku ya wakulima (nanenane) kanda ya ziwa Mhe. Magalula Saidi Magalula Mkuu wa Mkoa wa Geita watatu kutoka kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa sherehe hizo.Wakwanza kushoto ni ndugu Severine Kahitwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, wapili kutoka kushoto ni Mhe. Evarist Ndikilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Katika ufunguzi huo Mgeni rasmi alitoa wito kwa wananchi wote wa kanda ya ziwa kutembelea mabanda yote ili wakajifunze teknolojia mbalimbali zinazotumika  katika uzalishaji. Aidha, aliwataka wakulima wazalishe kwa tija kwa kutumia kanuni na mbinu bora za kilimo na mifugo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mazao yanayozalishwa ni bora na yanayokidhi mahitaji ya soko kwani biashara ya sasa ni ya ushindani.

Mgeni Rasmi wa ufunguzi wa sherehe ya siku ya wakulima (nanenane) kanda ya ziwa Mhe. Magalula Saidi Magalula Mkuu wa Mkoa wa Geita akihutubia wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo ambayo kikanda yalifanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Nyamuhongolo.

Wasanii maarufu wa kikundi cha maigizo cha jijini Mwanza Futuhi wakitoa burudani wakati wa kufungua siku ya wakulima(nanenane)kanda ya ziwa.


Wananchi mbalimbali wakitizama bidhaa katika mabanda ya halmashauri za Wilaya za Mkoa wa Geita. wakati huo wataalamu wakitoa ufafanuzi kuhusu bidhaa hizo kwa wananchi hao.


Wananchi wa Kanda ya Ziwa wakishuhudia uzinduzi rasmi wa maonyesho ya siku ya wakulima (nanenane) ambayo yalizinduliwa tarehe 5/08/2014 jijini Mwanza, Mgeni rasmi wa uzinduzi wa sherehe hizo alikuwa Mhe. Magalula S Magalula Mkuu wa Mkoa Geita.