MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Tuesday 24 February 2015

VIONGOZI WA MKOA, WILAYA NA HALMASHAURI ZOTE MKOANI GEITA WAPEWA SEMINA ELEKEZI

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akifungua semina elekezi ya viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya. Semina hiyo elekezi iliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa lengo la kuwaongezea uwezo viongozi wa Mkoa huu ili watekeleze majukumu yao ipasavyo, kukumbushana wajibu kama watendaji wakuu ndani ya Mkoa na kuchambua fursa na changamoto zilizopo katika Mkoa,kubainisha vipaumbele na kuweka mipango thabiti inayoweza kuharakisha maendeleo ya Mkoa wa Geita.
Picha tofautitofauti za Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita  wakati alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Uongozi na namna kiongozi anavyotakiwa kuwa katika utendaji wa shughuli za serikali na jamii.




Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita ndugu Charles Pallangyo akifafanua jambo mbele ya wajumbe (awapo kwenye picha) wakati wa uzinduzi wa semina elekezi ya viongozi wote wa serikali wa Mkoa wa Geita iliyofanyika hivi karibuni Mkoani hapa.

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita (wakwanza kulia) na Manzie Mangochie Mkuu wa Wilaya ya Geita katikati wakiwa katika Semina elekezi ya Viongozi wa Mkoa wa Geita.

Mwezeshaji kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ( SUA) Ndugu Joseph Massimba akiwasilisha Mada kuhusu uwezeshaji wa Vijana kupitia Kilimo wakati wa semina elekezi ya Viongozi Mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita Elisha Lupuga akichangia Mada wakati wa Semina Elekezi ya Viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya Mkoa wa Geita.

Viongozi wa Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Dhahabu Geita Gold Mine (GGML) wakiwa katika Semina elekezi ya viongozi Mkoani Geita iliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Nyankumbu na kuhudhuriwa na Taasisi za Umma na binafsi ikiwemo kampuni hiyo.


Viongozi mbalimbali wa Wilaya na Halmashauri za  Mkoa wa Geita wakiwa katika ukumbi wa mikutano wakati wa semina elekezi kwa viongozi  iliyofanyika Mkoani Geita kuanzia Tarehe 16-20/02/2015.