MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 21 January 2015

WANANCHI MKOANI GEITA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII ILI WAJILETEE MAENDELEO KATIKA JAMII YAO

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Igate wilaya ya Geita punde baada ya kufungua ghala la kuhifadhi matunda na mbogamboga la kijiji hicho ambalo limejengwa kwa msaada wa shirika lisilo la kiserikali ACCORD kwa ghalama ya Tshs milioni 53 kwa lengo la kuwasaidia wananchi wa kata za Nzera ,Bugando, Katoma ambao ni maalufu kwa kilimo cha Nanasi kuhifadhi na kuuza matunda hayo katika ghala hilo. Katika hotuba yake Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi hasa vijana kufanya kazi kwa bidii ili wajiletee maendeleo. Hata hivyo Mkuu wa Mkoa aliwaeleza wananchi kuwa serikali inafanya kila linalowezekana ili kuwatafutia wakulima wa zao la nanasi soko la ndani na nje ili kuwainua kiuchumi. Vilevile alisema kuwa serikali inatambua mchango wa zao la nanasi katika Mkoa wa Geita hivyo itaunda vikundi viwili vya mfano na kuviwezesha utaalamu, mbegu, mbolea na misaada mingine ili vianze kulima na kuzalisha nanasi kwa wingi na kuongeza kipato kwa vijana na jamii kwa jumla. Kijiji cha Igate kinalima jumla ya ekeri 769 ambazo uzalisha zaidi ya tani 27,600 kwa mwaka katika awamu tatu za mavuno ambapo kila awamu hutoa tani 9,228. Aidha katika kuhakikisha kuwa wananchi wanajiongezea kipato wamejiunga katika kikundi cha UWAMAMI ambacho mpaka sasa kina jumla ya wanachama 91 ambao wanatumia ekari 71 katika kilimo cha mbogamboga na ekari 283 katika kilimo cha nanasi.

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Ghala la kuhifadhi matunda na Mbogamboga kijiji cha Igate.


Viongozi mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya kiserikali wakimsikiliza kwa makini Mheshimiwa Mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa Ghala la kuhifadhi matunda na Mbogamboga Kijiji cha Igate.

Vikundi vya burudani vya ngoma za asili vikitumbuiza wakati wa ufunguzi wa ghala la kuhifadhi matunda na mbogamboga Igate.


Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita akifurahia na wananchi (hawapo kwenye picha) baada ya kuweka jiwe la ufunguzi katika ghala la kuhifadhi matunda na mbogamboga kijijini Igate.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa Fatma Mwassa akijionea namna shughuli za kuhifadhi na kuuza matunda na mbogamboga ndani ya Ghala zinzvyofanyika baada ya kufungua jengo hilo.

Mwakilishi wa kikundi cha wakulima wa nanasi Igate (UWAMAMI) akisoma taarifa ya kikundi hicho mbele ya Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita wakati wa ufunguzi wa ghala la kuhifadhi matunda na mbogamboga lililojengwa na na shirika lisilokuwa la kiserikali ACCORD kijijini Igale -kata ya Nzera Halmashauri ya wilaya Geita.

Tuesday 20 January 2015


Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akikagua Shamba la Mananasi la kikundi cha UWAMAMI kilichopo katika kijiji cha Igale  Kata ya Nzera Halmashauri ya Wilaya ya Geita.

Thursday 15 January 2015

WACHAMBUZI WA PAMBA MKOA WA GEITA WATAKIWA KUWAPELEKEA WAKULIMA WA PAMBA VIUADUDU(DAWA) KWA WAKATI

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa akifungua Mkutano wa wadau wa Sekta Ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita ambapo aliwataka wachambuzi wa Pamba kupitia umoja wao (UMWAPA) kutekeleza Kilimo cha Pamba Cha Mkataba kwa kusambaza Mbegu za Pamba pamoja na Viuadudu (dawa) ili kuepusha hasara kwa wakulima ambao wanalima Pamba lakini Pamba hiyo inashambuliwa na wadudu kwasababu ya makampuni ya ununuzi wa Pamba ambayo wanaingia nayo Mkataba yanachelewa kufikisha viuadudu hivyo kwa wakati. Aidha, katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa aliwataka wachambuzi hao kuhakikisha kuwa wanasambaza mbegu kwa ujazo  tofauti wa kuanzia kilo 50, 25 na 10 ili kuondoa malalamiko ya wakulima kupunjwa na mawakala wasio waaminifu. Mkoa wa Geita unatekeleza Kilimo cha Pamba cha Mkataba kwa kuwaunganisha wakulima wa zao hilo pamoja na Makampuni ya uchambuzi ambayo yanawakopesha pembejeo wakulima na baadae kurejesha gharama hizo kwa kuuza pamba kwa makampuni waliyoingia nayo mkataba. Kilimo hicho kwasasa katika Mkoa kinaanza kuonyesha mafanikio baada ya wakulima wengi kuingia katika utaratibu huo hivyo Mkoa unatarajia ongezeko la uzalishaji wa zao la pamba.



Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Bi. Husna Mwilima akichangia na kumshukuru Mgeni Rasmi wa Mkutano Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Fatma Mwassa kwa kumpatia nafasi ya kufunga Mkutano  huo muhimu kwa zao la Pamba.

Viongozi mbalimbali wa Serikali ngazi ya Mkoa na Halmashauri za Wilaya wakifuatilia kwa karibu Mkutano wa Wadau wa Sekta Ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita.

Kaimu Meneja wa Bodi ya Pamba Kanda ya Ziwa Bruma Kalidushi akitoa ufafanuzi juu ya ugawaji wa Pembejeo za kilimo cha Pamba katika Mkutano wa Wadau wa Sekta Ndogo ya Pamba Mkoa Wa Geita.

Mwakilishi wa Umoja wa Wachambuzi wa Pamba (UMWAPA) ndugu Mohamed Sharif akichangia wakati wa Mkutano wa Wadau wa Sekta ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita.


Mkulima wa zao la Pamba kutoka wilaya ya Nyang'hwale Mkoa wa Geita Masoud Mtolle akichangia mada wakati wa Mkutano wa Sekta ndogo ya wadau wa Pamba Mkoa wa Geita.
Wawakilishi wa Wakulima wa Pamba Mkoa wa Geita wakifuatilia mada wakati wa Mkutano.


Mkulima wa zao la Pamba Mkoani Geita Ndugu Emmanuel Shija akichangia mada katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita.



Wadau wa Sekta ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita wakiwa katika Mkutano uliofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita.