MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Tuesday 15 July 2014

"WANANCHI SAMINA WILAYA YA GEITA WATAKIWA KUFUATA SHERIA NA TARATIBU ZILIZOWEKWA NA NCHI"

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika eneo la Samina baada ya kutembelea eneo lililovamiwa na wachimbaji hao, katika Mkutano huo Mwenyekiti aliwataka wananchi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na kuacha tabia ya kuvamia maeneo ambayo yana leseni ili kutojiingiza katika migogoro isiyo ya lazima. Eneo la Samina ambalo limevamiwa na wachimbaji wadogo linamilikiwa kisheria na kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Geita Gold Mine (GGM). Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliwataka wananchi wasifanye vurugu katika maeneo yenye leseni wakati serikali ikifanya utaratibu wa kuwatafutia maeneo ambayo wataendesha shughuli zao za uchimbaji mdogo.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Wataalamu wa Madini Mkoa wa Geita wakitizama namna wachimbaji wadogo wanavyoendesha shughuli za uchimbaji katika eneo la samina eneo ambalo limevamiwa na wachimbaji hao.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita wakikagua eneo la Samina ambalo limevamiwa na wachimbaji wa madini wadogo wadogo.

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita wakiwa katika Mkutano wa hadhara ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo alikuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika eneo la Samina hivi karibuni.

Monday 14 July 2014

JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA LAKABIDHIWA PIKIPIKI 20 NA BAISKELI 4

Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi akikata utepe katika pikipiki 20 na Baiskeli 4 zilizotolewa na Kikundi cha wafanya biashara katika Mji wa Geita kwa lengo la kurahisisha kazi ya Askari Polisi katika kupambana na vitendo vya uharifu hasa katika maeneo yasiyopitika.Msaada huo kutoka kwa wafanya biashara umekuja baada ya Askari Polisi kwa kushirikiana na wananchi kufanikiwa kuwakamata majambazi wanaohusika na unyanganyi wa kutumia silaha.katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa aliwataka wananchi wote Mkoa wa Geita kuhakikisha kuwa wanatoa taarifa kwa jeshi la polisi kuhusu vitendo vinavyohusu uvunjifu wa amani.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Magalula Saidi akimkabidhi  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo pikipiki 20 zilizotolewa na kikundi cha wafanya biashara Mjini Geita.

Mwenyekiti wa kikundi cha wafanya biashara Mjini Geita Ndugu Bugomola akimkabidhi Mkuu wa Mkoa Pikipiki 20 kwa ajili ya jeshi la polisi Mkoa wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akiwasha pikipiki zilizotolewa na kikundi cha wafanya biashara kwa jeshi la polisi Mkoa wa Geita.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki jeshi la Polisi Mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa Ulinzi shirikishi Mkoa wa Geita Atanazy Enyasi akimkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi zawadi  kwa ajili ya askari waliofanya kazi nzuri ya kupambana na majambazi Mkoani Geita hivi karibuni.

Katibu Tawala Mkoa wa Geita ndugu Severine Kahitwa akizungumza katika hafla ya kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi Mkoa wa Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo akieleza jambo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na kikundi cha wafanya biashara  wa Mji wa Geita  ya kukabidhi pikipiki kwa jeshi la polisi Mkoani hapa.

Katibu wa kikundi cha wafanya biashara Mjini Geita ndugu Komba Otmary akisoma Risala ya kikundi wakati wa hafla ya kukabidhi pikipiki 20 kwa jeshi la Polisi na baiskeli 4 kwa Polisi jamii.

WILAYA YA BUKOMBE YATOA MAFUNZO YA WALIMU KATIKA KATA ZOTE

Afisa Elimu Mkoa wa Geita Ephrasia Buchuma akifunga mafunzo ya Walimu wa Wilaya ya Bukombe.Jumla ya Walimu 65 kutoka kata zote za wilaya ya bukombe walipatiwa mafunzo ya namna ya kumuandaa mwanafunzi ili ajue kusoma,kuhesabu na kuandika, lengo kuu likiwa ni kuboresha kiwango cha ufaulu katka Wilaya hiyo.Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Afisa Elimu wa Mkoa aliwapongeza viongozi wa Wilaya hiyo kwa uamuzi wao wa kutoa mafunzo hayo ambayo yanamwezesha mwalimu kwenda na wakati katika utoaji wa elimu bora kwa wanafunzi ili kuendana na malengo ya matokeo makubwa sasa.

Afisa Elimu Mkoa wa Geita akizungumza na Walimu wa Wilaya ya Bukombe waliohudhuria mafunzo ya Walimu.

Afisa Elimu wa Wilaya ya Bukombe akizungumza na walimu wa wilaya hiyo waliohudhuria mafunzo kabla ya kumkaribisha Afisa Elimu wa Mkoa wa Geita Bi. Ephrasia Buchuma ili afunge mafunzo ya siku tatu ya walimu.

Walimu mbalimbali kutoka kata za wilaya ya Bukombe wakiwa katika mafunzo wilayani humo hivi karibuni.