MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Friday 14 February 2014

BARAZA LA WAFANYAKAZI MKOA WA GEITA LAZINDULIWA RASMI NA MKUU WA MKOA WA GEITA Mh. MAGALULA S. MAGALULA NA WAJUMBE KUFANYA KIKAO CHAO CHA KWANZA.

Mgeni rasmi wa Baraza la wafanyakazi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita  Mh. Magalula Said Magalula akihutubia Baraza hilo baada ya kulizindua tarehe 12/02/2014, kushoto ni Katibu Tawala Mkoa wa Geita BW. Severine Kahitwa ambaye pia ndiye M/kiti wa Baraza hilo na kulia ni katibu wa TUGHE Mkoa wa Geita Bw. Samweli M. Magero uzinduzi huo ulifanyiaka katika ukumbiwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  Geita.





Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh. Magalula Said Magalula wa pili kutoka kulia akimsikiliza mjumbe wa BARAZA la Wafanyakazi Mkoani Geita alipokuwa mgeni rasmi na kuzindua rasmi BARAZA hilo mnamo tarehe 12/02/2014 ,kushoto ni Katibu  wa Baraza hilo na Mkuu wa kitengo cha Sheria Bw. Manase Ndoroma aliyechaguliwa na wajumbe kutoka kwenye majina yaliyopendekezwa na M/kiti wa Baraza hilo wa ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa wa Geita BW. Severine Kahitwa wa pili kutoka kushoto na kulia ni katibu wa TUGHE Mkoa wa Geita Bw. Samweli M. Magero, uzinduzi huo ulifanyika kaika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita.

KATIBU TAWALA




M/kiti wa BARAZA la wafanyakazi na RAS Geita bw. Severine Kahitwa katikati kulia ni Katibu wa TUGHE Mkoa wa Geita bw. Samweli M . Magero na kushoto ni Katibu wa BARAZA hilo bw. Manase Ndoroma ambaye pia ni Mkuu wa kitengo cha sheria ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita .  


Kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Utwala na Rasilimali Watu Bw. E.T. RUGARABAMU na kushoto ni Afisa Utumishi Bw. Magange Khamis Mwita katika kikao cha BARAZA la wafanyakazi lililozinduliwa jana 12/02/2014 na Mh. Mkuu wa Mkoa Said Magalula Mkoani Geita



Wajumbe wa Baraza la wafanyakazi Mkoa wa Geita wakiwa katika kikao cha uzinduzi wa baraza uliofanyika Mkoani Geita katika ukumbi wa Mkuu wa mkoa  jana 12/02/2014.

Viongozi na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wakiwa katika kikao baada ya uzinduzi rasmi wa baraza hilo jana tarehe 12/02/2014.




Mkuu wa Seksheni ya Mipango na Uratibu akiwasilisha Ukomo wa bajeti kwa mkoa wa Geita katika baraza la wafanyakazi lililozinduliwa jana na Mkuu wa Mkoa wa GEITA. 



Mbele kabisa ni Katibu Tawala Msaidizi Seksheni ya Serikali za Mitaa ambaye pia alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la wafanyakazi Mkoa wa Geita  Bib.Sania Mwangakala  akifuatilia jambo na wajumbe wengine katika uzinduzi huo wa Baraza la wafanyakazi uliofanyika katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Mkoani Geita tarehe 12/02/2014.

Thursday 13 February 2014



Baadhi ya wajumbe waliohudhuria  Baraza la wafanyakazi Mkoa wa Geita mnamo tarehe 12/02/2014 katika kikao cha uzinduzi wa Baraza hilo 

Friday 7 February 2014

PICHA ZA MATUKIO YA SHEREHE YA KUUAGA MWAKA 2013 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2014 ILIYOFANYIKA TAREHE 10/01/2014 MKOANI GEITA.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula S. Magalula akihutubia wakati wa Sherehe ya kuuaga Mwaka 2013 na kuukaribisha Mwaka 2014 zilizofanyika katika ukumbi wa Desire Park Mjini Geita
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Sherehe ya kuuaga Mwaka 2013 na kuukaribisha Mwaka 2014 Bw.Erasmusi Rugarabamu akikabidhi keki maalum kwa ajili ya Sherehe kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita.