MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Friday 11 November 2016

PSPF MKOA WA GEITA WACHANGIA MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA TSHS 7.5 MILIONI MKOANI GEITA

Edward Temu Kaimu Mkurugenzi wa PSPF Mkoa wa Geita  akikabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi 7,500,000/= kwa Mheshimiwa Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mji Geita. Mkuu wa Mkoa amewashukuru PSPF kwa mchango wao huo wenye manufaa katika Sekta ya Elimu Mkoani Geita na ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wadau wote wa maendeleo kuendelea kuchangia madawati ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wote katika Mkoa wa Geita wanakaa kwenye madawati wakati wa masomo yao katika shule zote za Msingi na Sekondari. Madawati yote yaliyopokelewa yamepelekwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ili kupunguza uhaba huo katika Halmashauri hiyo. 

Mwenyekiti wa kamati ya Madawati Mkoa wa Geita Atanazy Enyasi akizungumza na ndugu  Elias Kayandabila Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe baada ya kumkabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi 7.5 Milioni ikiwa ni mchango wa shirika la PSPF Mkoa wa Geita.

Viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoa wa Geita wakiwa wamekaa pamoja na wanafunzi kwenye madawati 100 yaliyotolewa na PSPF Mkoa wa Geita.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Selestine Gesimba akisisitiza jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 100 iliyoandaliwa na PSPF Geita. Ndugu Gesimba amewashukuru wadau wote wanaondelea kutekeleza ahadi yao walio ahidi wakati wa harambee ili kukamilisha na kumaliza tatizo la madawati katika Mkoa wa Geita.

Mheshimiwa Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akikabidhi madawati 100 kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati Mkoa wa Geita ndugu Atanazy Enyasi na Ernest Nyororo. Madawati hayo kutoka PSPF yamekabidhiwa kwa Halmashauri ya Mbogwe.


Mzee Atanazy Enyasi Mwenyekiti wa kamati ya madawati Mkoa wa Geita akizungumza  na kuwaomba wananchi na wadau wengine wa maendeleo kujitokeza na kuchangia madawati wakati wa hafla fupi ya Mkoa wa Geita kupokea madawati 100 kutoka katika mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSPF Geita.

Wanafunzi wakiwa wamekalia sehemu ya madawati iliyochangwa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF

Mheshimiwa Meja Jenerali (Mst) Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Geita walioshiriki katika hafla fupi ya kukabidhi madawati  100 iliyoandaliwa na PSPF Geita katika viwanja vya Halmashauri ya Mji Geita.