MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 19 August 2015

MWENGE WA UHURU 2015 WAZINDUA, KUFUNGUA NA KUWEKA MAWE YA MSINGI KATIKA MIRADI YA MAENDELEO 67 YENYE THAMANI YA TSHS. BILIONI 4,464,623,474/= MKOANI GEITA.

Askari na wananchi wa Mkoa wa Geita kwa pamoja wakiukimbiza Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Mkoani Geita kuanzia tarehe 10/08/2015 hadi tarehe 16/08/2015. Mwenge ulikimbizwa katika Wilaya zote 5 za Mkoa wa Geita na katika Halmashauri za Wilaya 6 kwa umbali wa Kilometa 664.13 katika miradi 67 ya maendeleo yenye thamani ya Tshs. Bilioni 4,464,623,474/=.

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Geita akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Nassoro Rufunga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga tarehe 16/08/2015 baada ya kutembelea, kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika jumla ya miradi ya maendeleo 67 ya Mkoa wa Geita. Miradi hiyo inathamani ya Tshs Bilioni 4,464,623,471/= fedha ambazo ni michango ya serikali kuu, wananchi, Halmashauri za Wilaya na Wahisani mbalimbali.

Mradi wa Tanki la maji Kilimahewa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ambao ulizinduliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru 2015 unaosaidia zaidi ya wananchi 2500 wa Ushirombo.

Mradi wa kisima kirefu cha Maji katika Kijiji cha Nyamalulu Halmashauri ya Wilaya Geita. Mradi huu ulizinduliwa na mbio za Mwenge 2015 hivyo kuwafanya wananchi wa kijiji hicho kupata maji safi na salama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa 2015 Juma Chum akizindua Trekta la Kijiji cha Nyamalulu Halmashauri ya Geita wakati wa mbio hizo wilayani Geita.Mradi huu unatarajia kusaidia wananchi katika usafirishaji wa mbolea mashambani na pia katika shughuli za kilimo kama vile kulima  maeneo makubwa hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao.


Baadhi ya wananchi na watumishi waserikali wakigusa Mwenge wa Uhuru ulipokuwa Mkoani Geita tarehe 10-16/08/2015.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge akimkabidhi mama Chandarua chenye dawa kuonyesha juhudi za serikali  za kupambana na ugonjwa wa malaria ili kuhakikisha kuwa wananchi wanakuwa na afya njema wakati wote.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2015 Juma Chum akikabidhi mzinga wa nyuki kwa kikundi cha wajasiliamali wanawake cha Ufugaji Nyuki wakati wa Mbio za Mwenge Mkoani Geita.Hii ni kuonyesha namna serikali inavyowasaidia wanawake ili waondokane na umaskini kwa kuwaunganisha katika vikundi ili wazalishe na kujipatia kipato.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2015 ndugu Juma Chum akizindua mradi wa maji bomba katika kijiji cha Kikumbaitare Halmashauri ya Wilaya Chato. Mradi huu utanufaisha watu zaidi ya 1500 ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2015 ndugu Juma Khatibu Chum akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa baada ya kuwasili Mkoa wa Geita, wengine katika mstari ni kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Geita.

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Chato manzie Mangochie baada ya Mwenge kuwasili Mkoani Geita ukitokea Mkoa wa Kagera na kupokewa katika kijiji cha Mkolani Wilaya ya Chato.

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita (aliye vaa suti nyeusi) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mheshimiwa John Mongella Mkuu wa Mkoa wa Kagera katika kijiji cha Mkolani Halmashauri ya Chato baada ya Mwenge kuwasili Mkoa wa Geita.

Msanii wa kikundi cha sanaa cha ngoma za asili akitumbuiza wakati wa mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Mkoani Geita tarehe 10/08/2015.