MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Thursday 19 June 2014

MATUKIO MBALIMBALI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA MKOA WA GEITA

Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Manzie Mangochie ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita akihutubia hadhara iliyojitokeza katika maadhimisho hayo amabapo aliwataka wazazi na walezi wa watoto kuhakikisha kuwa wanawapa watoto haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na Elimu na kuacha tabia ya kuwatumikisha watoto katika kazi ngumu. Aidha katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alitoa zawadi kwa wanafunzi watatu waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2013.


Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Geita wakiwa katika Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika wakwanza kutoka kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Ndugu Severine Kahitwa, wapili kutoka kulia ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Joseph Konyo na Kamishina wa uhamiaji Mkoa wa Geita Charles Washima.


Vikundi mbalimbali vya burudani vikitumbuiza wakati wa Maadhimisho ya Sherehe ya Siku ya Mtoto wa Afrika Mkoani Geita.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kasenga wakati wa maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika ambayo katika Mkoa wa Geita yalifanyika kijiji hicho wilaya ya Chato.



Watoto mbalimbali waliojitokeza kusherekea maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16/06/2014 wakiwa katika picha, ambapo katika Mkoa wa Geita Maadhimisho hayo yalifanyika katika kata ya Kasenga Tarafa ya Kachwamba Wilaya ya Chato.

Friday 13 June 2014

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Severine Kahitwa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili ofisi ya muda ya Tarafa ya Nyakamwaga wilaya ya Geita,lengo la ziara ya katibu Tawala wa Mkoa lilikuwa kukagua ujenzi wa Ofisi za Tarafa Mkoani Geita.

Mhandisi wa ujenzi ndg Edger Mungaya mbele ya Katibu Tawala wa Mkoa akitoa ushauri wa kiufundi kwa mkandarasi wa jengo.

Katibu Tawala Mkoa wa Geita akisaini kitabu cha wageni mala baada ya kukagua ujenzi wa Ofisi ya Tarafa ya Msalala Wilaya ya Nyang'hwale.

Majengo ya Ofisi za Maafisa Tarafa za Msalala wilaya ya Nyang'hwale na Kachwamba Wilaya ya Chato yanavyoonekana katika picha wakati ujenzi wake ukiendelea.

Thursday 12 June 2014

Katibu Tawala Mkoa wa Geita Severine Kahitwa wakwanza kulia akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa ujenzi wa Mkoa  ndg Edger Mungaya  katikati wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa Ofisi za Tarafa Mkoa wa Geita.

Katibu Tawala Mkoa wa Geita Severine Kahitwa akikagua ujenzi wa Ofisi ya Afisa Tarafa huko Wilayani Chato katika Tarafa ya Kachwamba.

Friday 6 June 2014

'' NI MARUFUKU KUKOPA PAMBA KUTOKA KWA WAKULIMA''

Mwenyekiti wa kikao cha wadau wa Sekta ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita akihutubia katika kikao cha sita cha sekta hiyo kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Geita.Kaika kikao hicho Mhe.Mkuu wa Mkoa aliyataka makampuni yote yanayonunua pamba ndani ya Mkoa wa Geita kutokopa Pamba kutoka kwa Wakulima.


Mkoa wa Geita umepiga marufuku kwa makampuni ya uchambuzi na ununuzi wa pamba kuacha tabia ya kukopa pamba kutoka kwa wakulima.

Akizungumza katika kikao cha sita cha wadau wa sekta ndogo ya pamba Mkoa wa Geita Mwenyekiti wa kikao hicho Magalula Saidi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita alisema kuwa ‘’ ni marufuku kwa kampuni yeyote ile inayonunua pamba katika Mkoa wa Geita kukopa pamba kutoka kwa wakulima kwani kufanya hivyo ni kumdumaza mkulima na kumcheleweshea maendeleo yake ya kila siku’’.

Mkoa wa Geita unatekeleza kilimo cha pamba cha mkataba ambapo wakulima wanakopeshwa pembejeo  bora kutoka kwa makampuni ili wazalishe kwa wingi na wanufaike na kilimo hicho.


Kikao cha sita cha wadau wa sekta ndogo ya pamba Mkoa wa Geita kilifanyika kwa lengo la kufanya tathimini ya kilimo hicho na changamoto zake kwa msimu unaokwisha 2013/2014 na pia kujadili namna  kilimo hicho kitakavyoendeshwa kwa msimu ujao.Hatahivyo wakulima wengi wa Mkoa wa Geita wanaonyesha kukubaliana na kilimo hicho ambacho inasemekana kina tija kwao.
Katibu Tawala Msaidizi Idara ya Uchumi na Uzalishaji Mkoa wa Geita Emil Kasagala akieleza mbele ya wadau namna  kilimo cha Mkataba cha pamba kinavyotekelezwa katika Mkoa wa Geita katika kikao cha kufanya tathimini ya kilimo hicho kwa  msimu unaokwisha na namna Mkoa ulivyojipanga kwa msimu mpya wa kilimo hicho.

Wadau wa Sekta ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita wakiwa katika kikao cha sita cha sekta hiyo kilicho kaa hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Geita, kikao hicho kilikaa kwa lengo la kufanya tathimini ya kilimo cha mkataba na changamoto zake kwa msimu wa 2013/2014.