MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 19 March 2014

WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA MKOA WA GEITA WATAKIWA KUWEKA UTARATIBU MZURI WA KUVIPELEKA VIKUNDI VYA WAFUGAJI NYUKI KWENDA KUJIFUNZA NAMNA YA UFUGAJI NYUKI BORA WILAYANI BUKOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akitundika mzinga wakati wa siku ya maadhimisho ya siku ya kutundika mizinga ambayo katika Mkoa wa Geita maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha Ikina kata ya Bukoli Wilaya ya Geita.

WAKURUGENZI GEITA WATAKIWA KUWEKA UTARATIBU MZURI KWA VIKUNDI KWENDA KUJIFUNZA UFUGAJI NYUKI WILAYA YA BUKOMBE:

Wakurugenzi  wa Halmashauri za wilaya Mkoani Geita wametakiwa kuweka utaratibu mzuri wa vikundi vya wafuga nyuki kwenda kujifunza namna bora ya ufugaji nyuki katika wilaya ya Bukombe ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika zao la nyuki.
Mwakilishi wa Wakala wa  Huduma za Misitu wilaya ya Geita ndg Bruno Kawiti akisoma risala katika maadhimisho ya siku ya ufugaji Nyuki iliyofanyika katika Kijij cha Ikina kata ya Bukoli Wilaya ya Geita.


Katibu wa kikundi cha ufugaji Nyuki cha Ikina Faustine Ntaliyo akisoma taarifa ya kikundi hicho mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi wa nne kutoka kushoto, wa kwanza kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Severine Kahitwa, wapili ni Katibu Tawala Msaidizi  Idara ya uchumi na uzalishaji ndg: Emil Kasagala na watatu ni Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Manzie Mangochie.

Mwenyekiti wa kikundi cha ufugaji Nyuki cha Ikina Bw; Eliusi Bupamba akieleza jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wakati wa maadhimisho ya siku ya utundikaji mizinga.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi wa nne kutoka kushoto mstari wa nyuma na wakwanza kutoka kulia mstari wa nyuma ni Katibu Tawala Mkoa wa Geita Bw Severine Kahitwa wakiwa katika picha ya pamoja na kikundi cha ufugaji Nyuki cha Ikina.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akitizama mzinga wa Nyuki baada ya kukamilisha zoezi la kutundika Mizinga hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Mhe. Manzie Mangochie akitambulisha wageni wakati wa maadhimisho ya siku ya utundikaji Mizinga ya Nyuki. 

Mmoja wapo wa mzinga wa Nyuki ambao umetundikwa katika msitu wa Ikina wakati wa maadhimisho ya siku ya utundikaji mizinga Mkoa wa Geita.

Monday 3 March 2014

MKUU WA MKOA ATEMBELEA WILAYA YA NYANG’HWALE

 

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi amefanya ziara  ya kikazi ya siku nne (4) wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita.

Wanafunzi wa shule ya sekondari Kafita

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Kafita alipotembelea shule hiyo hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Bukwimba Wilayani Nyang'hwale wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Magalula Saidi akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang'hwale.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi wa pili kutoka kulia akizungumza na watumishi wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani Nyang'hwale.

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza Amina Said wa shule ya sekondari Nyijundu akijibu swali lililoulizwa na Mkuu wa Mkoa Mhe.Magalula Saidi alipotembelea shule hiyo hivi karibuni.


Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Nyang'hwale Manzie Mangochie ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyijundu katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Mhe. Mkuu wa Mkoa Wilayani humo.


Shule ya Sekondari Nyijundu  ambayo ilitembelewa na Mkuu wa Mkoa,shule hiyo imejengwa kwa nguvu za wananchi kwa kushirikiana na serikali Wilayani Nyang'hwale.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Busolwa wakati wa ziara  ya kikazi wilaya ya Nyang'hwale hivi karibuni. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kukagua  utengenezaji wa madawati katika shule za msingi na pia kukagua upelekaji wa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari wilayani humo mwaka 2014.