Mheshimiwa Meja Jenerali (MST) Ezekiel E Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akisoma taarifa kwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu maeneo yaliyotengwa na Mkoa kwa ajili ya Shughuli za Uchenjuaji wa Miamba taka itakayotolewa katika Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM). Maeneo yaliyotengwa yamezingatia vigezo vya utunzaji wa mazingira pia afya za wananchi. Maeneo hayo ni pamoja na eneo la Lwenge Nyamikoma, Kasota "B'' (Halmashauri ya Wilaya Geita) na eneo la Samina ''B'' lililopo Halmashauri ya Mji Geita. Wananchi wametakiwa kuunda vikundi na kuvisajili ili kupatiwa miamba hiyo kwa kuwa haitatolewa kwa mtu mmoja mmoja. Zoezi hili ni utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa tarehe 31/07/2016 wakati wa ziara yake Mkoani hapa, pia ni juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi ili wajipatie kipato cha kuendesha maisha ya kila siku na kupata maendeleo.
|