MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Monday 15 August 2016

WAKAZI WA GEITA KUPATIWA MAGWANGALA (MIAMBA TAKA) KUTOKA MGODI WA GGM BAADA YA SERIKALI KUTENGA MAENEO YA SAMINA ''B'', LWENGE NYAMIKOMA NA KASOTA ''B''


Mheshimiwa Meja Jenerali (MST) Ezekiel E Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akisoma taarifa kwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu maeneo yaliyotengwa na Mkoa kwa ajili ya Shughuli za Uchenjuaji wa Miamba taka itakayotolewa katika Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM). Maeneo yaliyotengwa yamezingatia vigezo vya utunzaji wa mazingira pia afya za wananchi.  Maeneo hayo ni pamoja na eneo la Lwenge Nyamikoma, Kasota "B'' (Halmashauri ya Wilaya Geita) na eneo la Samina ''B'' lililopo Halmashauri ya Mji Geita. Wananchi wametakiwa kuunda vikundi na kuvisajili ili kupatiwa miamba hiyo kwa kuwa haitatolewa kwa mtu mmoja mmoja. Zoezi hili ni utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa tarehe 31/07/2016 wakati wa ziara yake Mkoani hapa, pia ni juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi ili wajipatie kipato cha kuendesha maisha ya kila siku na kupata maendeleo.


Mheshimiwa Sospeter Mhongo Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na Viongozi mbalimbali na Wadau wa Mazingira wa Mkoa wa Geita wakati wakati wakikagua maeneo ya kumwaga miamba taka kutoka Mgodi wa GGM. Kulia kwa Waziri ni Selestine Gesimba Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita na Kushoto ni Ali Kidwaka Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Geita.

Sunday 14 August 2016

Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Viongozi na wadau wa Mazingita Mkoa wa Geita wakikagua maeneo ambayo miamba taka (Magwangala) yatamwagwa kwa ajili ya Uchenjuaji wa Dhahabu kwa vikundi  vitakavyoundwa.