MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Tuesday 21 October 2014

MKOA WA GEITA WAZINDUA CHANJO YA SURUA-RUBELLA KWA WATOTO WA MIEZI 9 HADI CHINI YA MIAKA 15

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi Magalula akizindua chanjo ya Surua-Rubella kwa kumpa mtoto matone na dawa za minyoo huku akishuhudiwa na viongozi wengine wa serikali waliohudhulia ulinduzi huo uliofanyika katika kituo cha Afya Nyankumbu nje kidogo ya Mji wa Geita.Watoto 923,000 katika Mkoa wa Geita wanategemea kupata chanzo hizo.


Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi akiwahutubia wananchi wakati wa Uzinduzi Chanjo ya Surua - Rubella ambao ulifanyika katika kituo cha Afya Nyankumbu Halmashauri ya Mji wa Geita. Mhe Mkuu wa Mkoa alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wazazi na wanajamii kuwa Chanjo ni haki ya kila mtoto na ni jukumu la kila mzazi au mlezi kuhakikisha kuwa watoto wanapata chanjo na huduma nyingine muhimu za afya kama matone ya vitamini A na dawa za minyoo.Aidha alitoa angalizo kwa wananchi kuwa kuna kazi kubwa ya kuwaelimisha kuhusu kampeni ya chanjo ya Surua-Rubella ambayo inatolewa sanjali na huduma nyingine hivyo aliwataka wasaidiane na serikali kupeleka taarifa sahihi kwa wenzao ili kuepusha upotoshaji. ''Kila mmoja wetu anawajibu wa kuelimisha na kuhamasisha mwenzake ili tuweze kujitokeza kwa wingi wakati wa kampeni kwa kuwaleta watoto wote kupata chanjo kwa faida ya Afya zao ,Mkoa na Taifa''. Aliwataka wananchi kuwapeleka watoto katika vituo vya kutolea chanjo ili wakingwe dhidi ya magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na kuboresha maisha na afya zao.

Monday 20 October 2014

Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie akizungumza na wananchi wa Nyankumbu wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Surua - Rubella Mkoani Geita ambao ulifanyika katika kituo cha Afya Nyankumbu Halmashauri ya Mji Geita.


Wasanii wa kikundi cha ngoma za asili cha Bakomyalumi kutoka halmashauri ya Mji wa Geita wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Surua - Rubella Mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita mhe Magalula Saidi   wapili kutoka kulia akipata maelezo kutoka kwa mhudumu wa Afya namna shughuli za utoaji chanzo zinavyoendelea wakati wa uzinduzi wa chanjo hizo Mkoani Geita.Wakwanza kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Geita Dr.Kisala na watatu ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita ndugu Severine Kahitwa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe.Magalula Said Magalula wapili kutoka kulia kwa walio simama akijionea namna shughuli za utoaji chanjo, matone na dawa za minyoo  kwa watoto wa miezi 9 hadi chini ya miaka 15 zinavyoendelea wakati wa uzinduzi wa chanjo ya Surua- Rubella Mkoani Geita,wakwanza kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dr.Joseph Kisala.

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi Magalula akizungumza na akina mama waliojitokeza katika uzinduzi wa Chanjo ya Surua-Rubella ambao katika Mkoa wa Geita Uzinduzi huo ulifanyika katika Kituo cha Afya Nyankumbu Halmashauri ya Mji Geita.





Wananchi na watoto wa mtaa wa Nyankumbu Geita wakishuhudia burudani kutoka kwa msanii wa ngoma za asili wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Chanjo ya Surua-Rubella Mkoa wa Geita.

Wednesday 15 October 2014

''MKOA WA GEITA NA JUHUDI ZA UHAMASISHAJI WA UFUGAJI WA SAMAKI''

Afisa Uvuvi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita ndugu Tito Mlelwa wakwanza kulia pamoja na wafugaji wa Samaki wakiwa wameshika Samaki ambao wametokana na Ufugaji ambao unahamasishwa na Uongozi wa Mkoa kwa lengo la kuongeza kipato na kuleta maendeleo katika kaya na Mkoa.                                                                                              Ufugaji wa Samaki ni shughuli muhimu ambayo inasaidia katika kukuza uchumi katika kaya na Taifa, kwa kutambua hilo Mkoa wa Geita unahamasishwa Ufugaji wa Samaki kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini na ukosefu wa lishe bora kwa wananchi wake. Uhamasishaji huu unafanywa katika Wilaya zote tano (5) za Mkoa huu kupitia Idara ya Uchumi na uzalishaji. Mwaka 2013 kulikuwa na Mabwawa ya Samaki 33 kwa Mkoa mzima mpaka hivi sasa kuna jumla ya Mabwawa ya Samaki 92. Uhamasishaji wa kufuga Samaki unafanywa kwa wataalamu kuwatembelea wafugaji vijijini na kuwaeleza juu ya faida zitokanazo na Ufugaji wa Samaki pamoja na kuwapatia mbinu bora za Ufugaji wa Samaki. 


Afisa Uvuvi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita Tito Mlelwa wapili kutoka kulia akitoa ushauri wa namna ya utunzaji wa Bwawa la Samaki kwa wafugaji wa Samaki wilayani Chato.

Samaki wa kufugwa waliovuliwa kutoka katika mabwawa ya watu binafsi huko ipalamasa Wilaya ya chato baada ya uhamasishaji wa ufugaji wa Samaki unaofanywa na Mkoa wa Geita kwa lengo la kuinua kipato cha wananchi.

Friday 3 October 2014

MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJILI MKOANI GEITA WAKATI WA MBIO ZA MWENGE TAREHE 25/09/2014 HADI TAREHE 30/09/2014


Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi Magalula akisalimiana na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachael Kassanda baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili Mkoani Geita tarehe 25/09/2014 ukitokea Mkoa wa Mwanza.Ukiwa katika Mkoa wa Geita Mwenge wa Uhuru ulipitia jumla ya miradi 75 yenye thamani ya Tshs 8,087730919.5/=. Miradi hiyo ilijumuisha sekta mbalimbali kama maji, mifugo, kilimo, ujenzi, utawala, elimu, afya, ushirika, mazingira na biashara.Ukiwa katika Mkoa huu Mwenge ulikimbizwa umbali wa Km 701.01 kabla ya kukabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga tarehe 01/10/2014.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akipokea Mwenge wa Uhuru baada ya kuwasili Mkoani Geita.








Kiongozi wa Mwenge akijionea shughuli za ufuaji vyuma huko Bukoli Geita
Mkimbiza Mwenge kitaifa akizindua barabara ya mtaa huko Nyarugusu,barabara hiyo imejengwa kwa kiwango cha changalawe.
Uzinduzi wa barabara ya lami ya NMB,GESECO
Kiongozi wa mbio za Mwenge akiongea na wananchi wa Butobela baada ya kuzindua mashine ya kukamua alizeti ya kikundi cha vijana.
Kiongozi wa mbio za Mwenge akizindua Klabu ya kupinga Rushwa Bulela Sekondari

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Rachael Kassanda akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Geita wakati wa mbio hizo Mkoani humu ambapo aliwataka wananchi kuidumisha amani iliyopo  ili wazidi wajipatie maendeleo,pia aliwataka wananchi waepukane na vitendo vya Rushwa, Madawa ya kulevya pamoja na Ukimwi.

Wananchi wilayani Nyang'hwale wakiushangilia Mwenge wa Uhuru wakati ukiwasili katika kijiji cha Busolwa.

Kiongozi wa mbio za Mwenge akiweka jiwe la uzinduzi kwenye hifadhi ya mazingira katika Shule ya Sekondari Bukoli halmashauri ya wilaya ya Geita.

Kiongozi wa mbio za Mwenge akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa Nyumba 10 za watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Chato.

Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa akipampu maji punde baada ya kuzindua kisima kirefu cha maji Buhalahala Halmashauri ya Mji Geita.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Rachael Kassanda akifungua mradi wa maji katika kijiji cha msasa wilaya ya Bukombe. Mradi huu utanufaisha mamia ya watu ambao walikuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Rachael Kassanda akiweka jiwe la ufunguzi katika Nyumba ya Mganga hospitali ya Wilaya ya Bukombe.

Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Amani Mwenegoha akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Ibrahimu Marwa,Makabidhiano hayo yalifanyika katika kijiji cha Lulembela tarehe 30/9/2014. Katika kijiji hicho Mwenge wa Uhuru ulifungua mradi wa maji.

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe Ibrahimu Marwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mbogwe kabla ya kumwomba mkimbiza Mwenge kitaifa Ndugu Wito Mlemelwa kuweka jiwe la msingi katika Nyumba ya mwalimu wa shule ya Sekondari Mbogwe.

Wananchi wa kata ya Lugunga wilaya ya Mbogwe wakiwa wamejitokeza kwa wingi kuona na kuushangilia Mwenge wa Uhuru ambao ulifikishwa katani hapo kwa kazi ya kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya kata ya Lugunga wilayani humo.

Katibu Tawala Mkoa wa Geita Severine Kahitwa akiagana na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Rachael Kassanda wakati wa makabidhiano ya Mwenge kati ya Mkoa wa Geita na Mkoa wa Shinyanga huko Mwabomba.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Ndugu Severine Kahitwa akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Makabidhiano hayo yalifanyika tarehe 01/10/2014 katika kijiji cha Mwabomba mpakani mwa mikoa ya Geita na Shinyanga.