MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Thursday 26 March 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI ATEMBELEA MKOA WA GEITA WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WAWEKEZAJI ILI KUJILETEA MAENDELEO NA KUKUZA UCHUMI WA NCHI.

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya uchimbaji madini ya Geita Gold Mine (GGML) Michael Van Anen akimkabidhi waziri wa Nishati na Madini hundi ya  tshs bilioni 2.23 kama ushuru wa tozo (service levy) kwa halmashauri  ya Geita na halmashauri ya Geita mjini wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya mji wa Geita na kuhudhuriwa na viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali ,dini na binafsi.

Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini akiwakabidhi hundi ya Tshs bilioni 2.23 wenyeviti wa Halmashauri ya Geita na Halmashauri ya Geita Mjini. Fedha hiyo inatokana na kodi ya ushuru wa tozo (service levy) iliyolipwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Geita (GGML). Aliwataka Wenyeviti hao kuhakikisha kuwa fedha hizo zinafanya kazi za maendeleo na siyo vinginevyo ili kukuza uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Geita. Hata hivyo aliwaeleza wananchi kuwa watarajie kuona huduma bora zaidi kwenye elimu, afya, barabara, umeme na maji. Kampuni ya GGM imekuwa ikisaidia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa huu kama vile ujenzi wa shule,ujenzi wa nyumba za watumishi na kituo cha afya Nyakabale, maji na kituo cha ushauri nasaha Geita.

Mhe.Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na wananchi wa Mji wa Geita wakati wa Ziara ya Waziri wa  Nishati na Madini Mkoa Geita hivi karibuni.


Mhe. George Simbachawne Waziri wa Nishati na Madini akikagua shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu katika Mdodi wa Busolwa Mine wakati wa Ziara yake Mkoa wa Geita.
Mwekezaji wa ndani ambaye pia ni mmiliki wa kampuni ya uchimbaji wa madini ya Busolwa Mine Baraka Ezekiel akimwelezea waziri namna shughuli za uchimbaji wa madini zinavyofanyika katika Mgodi huo wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini Mkoa wa Geita. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni mhe Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita na Mhe.Agustino Maselle Mbunge wa Jimbo la Mbogwe Mkoa wa Geita.
Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa mgodi wa Busolwa Mine alipotembelea Mgodi huo Nyarugusu Mkoani Geita. Mstari wa Mbele waliokaa kutoka kilia  kwa Waziri wapili ni Agustino Maselle Mbunge wa Mbogwe, ndugu Charles Pallangyo Katibu Tawala Mkoa wa Geita na kushoto kwa waziri ni ndugu Baraka Ezekiel Meneja wa Busolwa Mine,Mhe.Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Geita na Mhe. Manzie Mangochie Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongozana na Mhe. George Simbachawene  Waziri wa Nishati na Madini wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya maji ambayo inatarajia kusambaza maji mjini Geita. Mradi huo wa maji wa Mjini Geita unatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya uchimbaji wa madini Geita (GGML). Mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema mei 2015.

Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini akikata utepe kuashilia kufungua nyumba 18 za wananchi wa Buhalahala ambazo zimejengwa na Mgodi wa Geita kama fidia baada ya kuchukua maeneo ya wananchi hao.Wapili kulia kwa Waziri ni Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita na kushoto ni Meneja wa Mgodi wa Geita Bw. Michael Van Anen.


Mhe.Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na wananchi wa buhalahala baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi kwenye nyumba 18 za wananchi hao.

Moja ya nyumba 18 ambazo zimewekwa jiwe la msingi la uzinduzi na Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini wakati wa ziara yake Mkoa wa Geita.Nyumba hii ina vyumba vitatu vya kulala ,sitting room, jiko na stoo.

Mhe.George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini akiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa buhulahala wilaya ya Geita baada ya kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa nyumba 18 za wananchi hao ambazo ni fidia kwao kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita baada ya kuhamishwa kutoka katika maeneo yao kupisha shughuli za uchimbaji madini.Viongozi wengine waliohudhuria katika tukio hilo ni Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhe. Manzie Mangochie Mkuu wa Wilaya ya Geita na Meneja wa mgodi wa Geita ndugu Michael Van Anen.


Wananchi wa Mkoa wa Geita hususani mjini Geita wakiwa wamejitokeza kwa wingi kumsikiliza Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku mbili Mkoa wa Geita.


Wednesday 11 March 2015

MKOA WA GEITA WAWAFARIJI WAANGA WA MAAFA YA MVUA KUBWA HUKO MWAKATA WILAYA YA KAHAMA



Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akimkabidhi Benson Mpesya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Gunia la mchele kuwakilisha bidhaa nyingine zilizotolewa na Mkoa wa Geita kwa wananchi wa kijiji cha Mwakata ambao walipatwa na maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa na upepo mkali na kupelekea watu zaidi ya 30 kupoteza maisha pamoja na uharibifu mkubwa wa mali za wananchi ikiwemo mifugo na makazi.Katika salamu zake Mkuu wa Mkoa alitoa rai kuwa msaada huo utumike kama ulivyokusudiwa na kuwafike walengwa.Aidha, aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali na wadau wengine wakiendelea na jitihada za kuwasaidia.Bidhaa zilizotolewa na Mkoa wa Geita ni pamoja na Mchele, Maharage, Unga n.k.Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Charles Pallangyo pamoja na wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Geita.


Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongea na wananchi wa Mwakata (hawapo kwenye picha) alipowatembelea kwa lengo la kutoa msaada na rambi rambi kwa waanga wa maafa ya mvua.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama ambaye pia ni muanga wa Mvua akimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Geita na ujumbe wake kwa   msaada walioutoa kwa wananchi wa kijiji hicho.

Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita katikati akijadiliana na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za Bukombe na Nyang'hwale aliokuwa ameambatana nao Mwakata - kahama.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita ndugu Charles Pallangyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukombe James Ihunyo (katikati) walipokuwa kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama.

Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Mwakata Wilaya ya Kahama wakimshuhudia Mkuu wa Mkoa wa Geita na ujumbe wake kutoka Mkoani Geita wakitoa rambi rambi na kuwajulia hali wananchi waliopatwa na maafa.



Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Benson Mpesya baada ya kuwasili kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama kwa ajili ya kutoa msaada na Mkono wa pole kwa waanga wa Mvua kali iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha vifo na uharibifu mali nyingi za wananchi wa kijiji hicho.




Gari kutoka Mkoa wa Geita likishusha bidhaa mbalimbali kwa ajili ya waanga wa maafa ya mvua na upepo mkali iliyonyesha hivi karibuni na kusababisha vifo, majeruhi na kuacha familia nyingi zikiwa hazina makazi huko Mwakata Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.