MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 27 January 2016

Mkurugenzi wa Mgodi wa Geita Gold Mine ndugu Terry Melpeter akizungumza na Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais wakati wa ziara yake Mkoani Geita.

Thursday 7 January 2016

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais akikagua moja ya wodi katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita.


Mheshimiwa Makamu wa Rais akimjulia hali mzazi baada ya kutembelea wodi ya wazazi na akina mama katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita. Akiwa katika hospitali hiyo aliwataka wakunga pamoja na madaktari kuhakikisha kuwa hakuna kifo chochote cha akina mama na watoto kinachotokea kwa sababu ya uzembe wa daktari au mkunga. Aidha, aliwataka akina mama kuhakikisha wanakwenda kijifungua katika hospitali kwakuwa kuna huduma nzuri kuliko majumbani na kwa wakunga wa jadi.

Mheshimiwa Makamu wa Rais akikagua Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita wakati wa ziara yake Mkoani hapa.


Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais akikata utepe  na kuweka jiwe la msingi  katika majengo ya wodi za huduma ya dharula (ICU) ambayo yalikarabatiwa na kuwekewa vifaa vipya kwa ajili ya huduma hizo.Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa na Waziri wa Afya Ummy Mwalimu wakwanza kushoto.

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasili katika viwanja vya hospitali Teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita kwa ajili ya Ukaguzi wa Hospitali hiyo, huku akiambatana na Viongozi mbalimbali wa serikali kutoka kushoto wapili ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Bi. Fatma Mwassa na kutoka kulia wapili ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Charles Pallangyo akisalimiana na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuwasili Mkoani Geita tarehe 04/01/2016.

Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wakiwa tayari kushiriki katika ziara ya Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akiwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita tarehe 4/01/2016 kwa ajili ya kusomewa taarifa ya Mkoa.(PICHA ZOTE OFISI YA MKUU WA MKOA GEITA)