MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Tuesday 2 February 2016

MHESHIMIWA SAMIA SULUHU MAKAMU WA RAIS AZINDUA WODI YA WAGONJWA WA DHARULA, MRADI WA MAJI, KIKUNDI CHA USHONAJI CHA AKINA MAMA NA VIJANA , MITAMBO YA UJENZI WA BARABARA MKOANI GEITA.

Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikabidhi Mashine ya Echo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Joseph Kisala alipotembelea Hospitali hiyo na kuzindua wodi ya wagonjwa dharula na wodi ya watoto. Mashine hiyo ni moja kati ya vifaa vya kisasa ambavyo vimewekwa katika Hospitali hiyo na serikali kwa lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora za Afya na kwa wakati. Aidha katika ziara hiyo Makamu wa Rais alizindua mitambo ya kuchuja maji Nyankanga na kituo cha maji Nyankumbu , Mradi huo utasaidia zaidi ya watu 4000 kupata maji safi na salama. Pia, alitembelea mradi wa ushonaji wa akina mama na vijana wa kikundi cha Nyakatoma ambao unalenga kuwaendeleza vijana na wanawake ili kujipatia maendeleo. Vilevile alizindua mitambo ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya tshs 2.1 bilioni fedha ambazo zilitokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Geita. Mitambo hiyo itasaidia kuboresha miundombinu ya barabara na kusidia kupunguza gharama katika mitambo ya kukodi na kuongeza kipato kwa Halmashauri hiyo.


Kikundi cha akina mama na vijana cha ushonaji Katoma kilichotembelewa na Makamu wa Rais.

Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa mitambo ya kuzalisha maji Nyankanga Geita Mjini ambayo itazalisha maji ya kutosha  watu zaidi ya 4000 itakapokamilika.Mradi huo unatekelezwa kati ya serikali na mgodi wa Geita Gold Mine kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama.

Makamu wa Rais akikata utepe wakati akizindua mitambo ya kuzalisha na kuchuja maji katika eneo la Nyamkanga Mradi huu utahudumia wananchi zaidi ya 4000.

Mitambo ya ujenzi wa barabara iliyonunuliwa na Halmashauri ya Mji Geita na kuzinduliwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Geita Max Kamaoni akisoma taarifa ya ununuzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ambayo ilizinduliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais yenye thamani ya Shilingi 1.2 bilioni fedha ambazo ni mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo. Makamu wa Rais alipongeza jitihada zilizofanyika mpaka kupata mitambo hiyo muhimu kwa maendeleo ya Halmashauri hata, hivyo aliagiza kuwa mitambo hiyo itunzwe na itumike kwa kazi zilizokusudiwa.

Mheshimiwa Makamu wa Rais akizungumza na wananchi wa Geita awapo kwenye picha wakati wa ziara yake Mkoani hapa.

Kwaya ya Yeriko AIC Geita ikitumbuiza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mkoani Geita.


Wananchi pamoja na watumishi wa idara ya Afya wa Mkoani Geita wakifuatilia kwa karibu maelekezo ya Mheshimiwa Makamu wa Rais wakati akizungumza nao hivi karibuni.

Mheshimiwa Makamu wa Rais akiongozana na viongozi mbalimbali wa kitaifa na Mkoa wa Geita wakati wa ukaguzi wa Hospitali Teule ya Mkoa. Kutoka kulia ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, kushoto ni Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita , mwingine ni Mhe. Vick Kamata (Mb).

Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa akijadili jambo na Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ziara yake Mkoa wa Geita.

Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi wakimsikiliza Mheshimiwa Makamu wa Rais hayupo pichani wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani Geita.