MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 16 April 2014

MKOA WA GEITA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

Serikali Mkoa wa Geita imejidhatiti kuboresha hali ya Elimu katika Mkoa kwa kuboresha miundombinu ya shule na usimamizi makini.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi wakati akiwahutubia wadau wa Elimu Mkoa wa Geita katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya wasichana ya Nyankumbu Mkoani hapa.

"Miundombinu ya shule katika shule za Msingi na Sekondari siyo ya kuridhisha hasa upungufu wa madawati katika shule za msingi Wito wangu kwenu ninyi wadau ongezeni jitihada ya kuwahamasisha wananchi kutengeneza madawati ili kupunguza tatizo hili katika shule zetu.Halmashauri zikumbuke kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hasa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo kwa ajili ya shule za msingi na sekondari" alisema Mkuu wa Mkoa.

Wadau wa elimu Mkoa wa Geita walikutana pamoja ili waone namna ya kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha hali ya elimu katika Mkoa.

Mkoa wa Geita umepiga hatua katika uandikishaji wa wanafunzi wa awali ambapo kwa mwaka 2014 asilimia 79.4% ya wanafunzi wameandikishwa, kwa darasa la saba ni 91%.Mwenendo wa kuripoti shuleni kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ni asilimia 84%.Wito umetolewa kwa wadau wote kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaripoti shule haraka iwezekanavyo, na wazazi wote ambao hawajapeleka watoto wao shule wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

Katika kuhakikisha kuwa tatizo la mdondoko mkubwa na utoro unaozikabili shule za mkoa wa Geita unakomeshwa wadau wametakiwa kuhakikisha watoto walioripoti shuleni wanahudhuria kila siku bila kukosa.
Magesa Jumapili:


Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Severine Kahitwa akifungua kikao cha wadau wa Elimu Mkoa wa Geita, Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana Nyankumbu mjini Geita.

Afisa Elimu wa Mkoa wa Geita Bi; Ephrasia Buchuma akiwasilisha mada wakati wa kikao cha wadau wa Elimu Mkoa wa Geita.

Wadau wa Elimu Mkoa wa Geita wakiwa katika kikao ambacho kilifanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Nyankumbu.

Wadau wa Elimu Mkoa wa Geita wakitembea kujionea namna ujenzi wa shule ya Wasichana Nyankumbu unavyoendelea wakati wa kikao cha wadau wa Elimu Mkoa wa Geita Mbele kulia ni Mhe. Magalula Saidi Mkuu wa Mkoa wa Geita na katikati ni Mkuu wa shule ya Sekondari Nyankumbu.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Nyankumbu wakisoma shairi wakati wa kikao cha wadau wa Elimu Mkoa wa Geita kilipofanyika shuleni hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi akipanda mti wa kumbukumbu wakati wadau wa elimu Mkoa wa Geita walipotembelea shule ya sekondari Nyankumbu.


Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Nyankumbu ambao walikuwa wakifanya utafiti katika maabara ya shule hiyo.

Mwanafunzi wa Kidato cha tatu shule ya Sekondari Nyankumbu Eliza Abeli akielezea kwa wadau wa Elimu  namna ya kuchanganua sentensi  walipoitembelea shule hiyo hivi karibuni.Aliye mbele ni Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe Magalula.

Msimamizi wa Ujenzi wa Nyumba za Walimu na Mabweni ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyamkumbu akieleza jambo kwa wadau wa Elimu wakati walipofanya ukaguzi katika shule hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Geita Manzie Mangochie wapili kutoka kulia akimwongoza Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Saidi wakwanza kushoto wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankumbu Mkoa wa Geita.Katikati ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ni Bi Husna Mwilima Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe.

Wadau wa Elimu Mkoa wa Geita wakiwa katika moja ya Nyumba za walimu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Nyankumbu muda mfupi baada ya kukagua ujenzi huo ambao unadhaminiwa na Mgodi wa Geita Gold Mine.Walio mstari wa kwanza kutoka kushoto wakwanza ni katibu Tawala wa Mkoa Bw; Severine Kahitwa, wapili ni Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Amani Mwenegoha na wa tatu ni Mkuu wa Mkoa wa Geita  Mhe Magalula Saidi.