MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Friday 10 July 2015

FAHAMU YALIYOJILI MKOANI GEITA WAKATI WA UFUNGUZI WA TAMASHA LA LIVE YOUR GOALS NA MAFUNZO YA GRASSROOTS YALIYOANDALIWA NA TFF PAMOJA NA FIFA

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Geita akizumgumza na wadau wa mpira wa miguu wa wanawake pamoja na wananchi (hawapo katika picha) wakati wa ufunguzi wa Tamasha la  LIVE YOUR GOALS na Mafunzo ya Grassroots kwa walimu wa shule za msingi yaliyofanyika katika Mkoa wa Geita kwa lengo la kuhamasisha watoto wa kike kushiriki katika mpira wa miguu.  Katika Tamasha hilo mheshimiwa Fatma Mwassa alitoa rai kwa wazazi wote kuona umuhimu wa kuwaruhusu watoto wao wa kike kushiriki katika michezo hususani mpira wa miguu kwakua michezo ni fursa na inasaidia kujenga mwili na akili na pia kuna fursa nyingi za kimaendeleo.  Pia aliwapongeza walimu wote waliopata mafunzo hayo na kuwataka kutumia ujuzi huo kwa faida ya mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla. "Nafahamu kuwa walimu kutoka wilaya zote na Halmashauri sita za Mkoa wa Geita wameshiriki ipasavyo katika mafunzo haya, ni imani yangu taaluma hii itafika katika shule zote za Mkoa wa Geita ili kufanya program hii kuwa endelevu''.  Hata hivyo aliwapongeza FIFA na TFF kwa kuuchagua Mkoa wa Geita kuwa wakwanza katika kutekeleza program hii ambapo aliahidi kuanzisha mashindano mengine katika Mkoa yatakayojulikana kwa jina la Blatter Cup (IF YOU DO FIFA DOES)

Ndugu Henry Tandau Mkurugenzi wa ufundi na utawala wa shirikisho la mpira wa miguu duniani (FIFA) akimkabidhi mgeni rasmi Bi: Fatma Mwassa zawadi ya mipira wakati wa ufunguzi wa Tamasha la LIVE YOUR GOALS lililofanyika shule ya Sekondari Nyankumbu Mkoani Geita.

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akikabidhi zawadi ya mipira kwa mmoja wa washiriki baada ya kufanya vizuri katika Tamasha, kushoto ni Mheshimiwa  Manzie Mangochie Mkuu wa wilaya ya Geita.

Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya mpira wa wanawake kutoka TFF Ndugu Kiondo akizungumza na wadau wa mchezo wa mpira wa miguu Mkoani Geita wakati wa ufunguzi wa Tamasha la LIVE YOUR GOALS.

Thursday 9 July 2015

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Geita (GEREFA) Salum Kulunge akizungumza kuhusu maendeleo ya mpira wa miguu ndani ya Mkoa wa Geita wakati wa ufunguzi wa Tamasha la LIVE YOUR GOALS na Mafunzo ya Grassroots Mkoani Geita.

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha mpira wa miguu Geita (GEREFA) na mabalozi wa mchezo wa mpira wa wanawake nchini. Wanne kutoka kushoto ni Mheshimiwa Manzie Mangochie Mkuu wa Wilaya ya Geita.

Mheshimiwa Fatma A. Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita ( mstari wa kwanza aliyevaa Tshirt nyeupe katikati ya watoto) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wakike walioshiriki katika tamasha la LIVE YOUR GOALS Mkoani Geita.

Baadhi ya watoto wakike wakicheza mpira wa miguu katika viwanja vya shule ya sekondari ya wasichana Nyankumbu wakati wa ufunguzi wa Tamasha la LIVE YOUR GOALS na mafunzo ya Grassroots Mkoani Geita. Mafunzo hayo yaliandaliwa na TFF pamoja na FIFA.

Monday 6 July 2015


Baadhi ya washiriki wa Tamasha la LIVE YOUR GOALS kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Geita wakiwasili katika viwanja vya michezo Nyankumbu Mkoani Geita.

Baadhi ya wanamichezo na wadau mbalimbali wa michezo waliojitokeza kushuhudia Ufunguzi wa Tamasha la LIVE YOUR GOAL na Mafunzo ya Grass Roots kwa Mpira wa wanawake uliofanyika  katika  uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Nyankumbu Wilaya ya Geita.