Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akifungua semina elekezi ya viongozi wa Mkoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya. Semina hiyo elekezi iliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita kwa lengo la kuwaongezea uwezo viongozi wa Mkoa huu ili watekeleze majukumu yao ipasavyo, kukumbushana wajibu kama watendaji wakuu ndani ya Mkoa na kuchambua fursa na changamoto zilizopo katika Mkoa,kubainisha vipaumbele na kuweka mipango thabiti inayoweza kuharakisha maendeleo ya Mkoa wa Geita.Katika ufunguzi huo Mhe; Fatma Mwassa alizitaka halmashauri zote za Wilaya Mkoani Geita kuhakikisha kuwa katika mwaka huu wa fedha ziandae mpango wa muda wa kati wa matumizi (Medium Term Expenditure Frame Work) kwa kuzingatia vipaumbele muhimu vinavyokubalika na vitakavyoongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani.Semina hiyo ya siku tano ilijumuisha wadau mbalimbali ambao walikuja kutoa uzoefu wao kwa Mkoa wa Geita, wadau hao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Sokoines (SUA), Chuo Kikuu cha Ardhi (UCLAS),Sekretariet ya Mkoa wa Tabora, Mgodi wa Geita Gold Mine,TAKUKURU na Sekretariet ya Maadili ya Viongozi. | |
|