Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete amewataka viongozi na wazazi Mkoa wa Geita kuhakikisha kuwa wanafunzi wote walioacha masomo kwasababu mbalimbali wanatafutwa na kurudishwa shuleni.
Katika
hotuba yake ya kuzindua Mkoa wa Geita na mpango mkakati wa Mkoa katika uwanja
wa michezo wa Kalangalala Rais Kikwete amesema kuwa idadi ya wanafunzi
wanaoandikishwa kuanza shule ni kubwa kuliko wanafunzi wanaohitimu masomo
katika mkoa wa Geita hivyo ni lazima serikali serikali ifanye jitihada kubwa.
Mhe
Rais anasema ‘’Viongozi wa Mkoa na
Halmashauri hakikisheni watoto wote walioacha masomo wanatafutwa popote walipo
kwa kuunda sheria ndogondogo zinazowabana wazazi ili watoe msukumo kwa watoto wao kwenda shule tusipofanya hivyo
tutakuwa na Mkoa wenye wananchi wengi wasiojua kusoma na kuandika na hivyo
kuchelewesha maendeleo’’.
Aidha
katika mkutano huo Mhe. Rais amekabidhiwa hundi ya shiringi 25 millioni kutoka
Benki ya NMB ikiwa ni sehemu ya mchango wa kusaidia huduma za afya katika mkoa
wa Geita.
Katika
ziara hiyo ya siku tano ndani ya Mkoa wa Geita Rais Kikwete anatarajia kuweka
mawe ya msingi katika miradi mitatu ya
maendeleo inayotekelezwa na serikali ukiwemo ujenzi wa barabara mbili kwa
kiwango cha lami za Bwanga-Biharamulo urefu 67 KM na Bwanga-Uyovu urefu 45 KM,na ofisi ya CCM Chato, Kufanya
mikutano ya hadhara saba katika maeneo mbalimbali, kufungua miradi miwili ya
maendeleo ya Ng’anzo shule ya msingi na zahanati ya Kasota.
Pia Mhe.Rais Kikwete atazindua miradi mitano ya maendeleo ikiwemo mradi mmoja (1) wa maji katika kijiji cha Nyakafuru, kuzindua miradi miwili ya uchenjuaji wa dhahabu katika maeneo ya Nyamigogo na Katente katika wilaya za Nyang’hwale na Mbogwe, kuzindua mradi wa umeme huko Katoro –Geita na Wodi ya akina mama.
Aidha
Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atatembelea na kukagua miradi
miwili ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Theatre katika kituo cha afya Iboya na
Mgodi mdogo wa Baraka Gold Mine huko Nyaruyeye wilaya ya Geita.