MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Sunday 24 April 2016

MKUU WA MKOA WA GEITA MEJA JENERALI EZEKIEL KYUNGA ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA NYUMBA 18 ZA WATUMISHI, HOSPITALI TEULE YA MKOA WA GEITA NA SOKO LA WAKULIMA NYANKUMBU HALMASHAURI YA MJI GEITA


Mheshimiwa Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa Geita akizungumza na mjasiliamali wa kuuza viazi vitamu Bi. Aneth Mabula katika Soko la wakulima Nyankumbu Halmashauri ya Mji Geita alipotembelea soko hilo hivi karibuni. Akiwa sokoni hapo Mkuu wa Mkoa alisisitiza suala la usafi katika maeneo yote ya Soko. Aidha aliwaeleza wafanya biashara kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha ina boresha soko hili ili wananchi wafanye biashara katika mazingira mazuri na salama kwa afya za wateja wao.


Katika ziara hiyo Mkuu wa pia alipata fursa ya kutembelea Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita kwa lengo la kuona namna huduma kwa wananchi zinavyotolewa katika Hospitali hiyo. Aidha, alipongeza juhudi za kampuni ya Mgodi wa Geita (GGML) Katika kusaidia kuboresha huduma za afya kwa kununua vifaa vya kisasa.  Hata hivyo aliwataka watumishi wa Idara hiyo kufanya kazi kwa weledi ili kutatua matatizo ya wananchi wanaofika katika Hospitali hiyo kupata Huduma.