MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 1 January 2014

MATOKEO DARASA LA SABA


KIWANGO CHA UFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA CHAONGEZEKA MKOA WA GEITA.

Wanafunzi 29383 waliomaliza elimu ya msingi wakiwemo wavulana 14535 na wasichana 14848 wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani mkoani Geita.
Akitangaza matokeo hayo,kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita ,Bw.

Emili Kasagala alisema kuwa idadi hiyo ni sawa na asilimia 52 ya wanafunzi  waliofaulu.

Alisema kuwa matokeo hayo ya Mkoa ni wastani wa matokeo ya wilaya zote za Mkoa wa Geita ambapo kuna ongezeko dogo la ufaulu ukilinganisha na mwaka jana ambapo kulikuwa na wastani wa asilimia 31.
 Katika kutekeleza mpango wa matokeo makubwa sasa,mwaka huu ilitakiwa kiwango cha ufaulu kifikie asilimia 60 ya watahiniwa wote.

Alisema Mkoa wa Geita haujafikia asilimia hiyo hivyo jitihada zaidi zinahitajika kuhakikisha kuwa mwakani wanaongeza ufaulu zaidi kwani kwa sasa nafasi ya kitaifa Mkoa wa Geita ni wa 10 kati ya Mikoa yote ya Tanzania bara.

Kwa upande wake Ofisa Elimu Mkoa Bi. Ephrasia Buchuma alisema kiwango cha asilimia 52 hakiridhishi sana hivyo aliwataka maafisa Elimu wa wilaya kuhakikisha kuwa wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara katika shule zote na wakaguzi wawezeshwe kukagua shule, kuhakikisha kuwa ratiba ya masomo kwa mujibu wa sheria ya Elimu unazingatiwa, kuchukua hatua kwa walimu na wanafunzi watoro kwa mujibu wa sheria , kutenga muda kwa ajili ya KKK na kutoa chakula cha mchana kwa wanafunzi.Haya yakifanyika basi hali ya ufaulu itakuwa nzuri na malengo ya mpango wa matokeo makubwa sasa utafanikiwa.
Ufaulu kiwilaya unaonyesha kuwa Geita Mjini ni 66%, Bukombe ni  59%, Chato 58%, Mbogwe 49%, Geita 45% na Nyang’hwale ni 41%.

Aidha Afisa Elimu Mkoa alisema kuwa Mkoa una jumla ya wanafunzi 6 wenye mahitaji maalum ambao wote watapangiwa  Shule na WEMU kwa kuzingatia ulemavu wao.

Na: Magesa Jumapili.