Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika eneo la Samina baada ya kutembelea eneo lililovamiwa na wachimbaji hao, katika Mkutano huo Mwenyekiti aliwataka wananchi kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na kuacha tabia ya kuvamia maeneo ambayo yana leseni ili kutojiingiza katika migogoro isiyo ya lazima. Eneo la Samina ambalo limevamiwa na wachimbaji wadogo linamilikiwa kisheria na kampuni ya uchimbaji wa dhahabu ya Geita Gold Mine (GGM). Katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama aliwataka wananchi wasifanye vurugu katika maeneo yenye leseni wakati serikali ikifanya utaratibu wa kuwatafutia maeneo ambayo wataendesha shughuli zao za uchimbaji mdogo.