Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Geita akikabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Nassoro Rufunga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga tarehe 16/08/2015 baada ya kutembelea, kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika jumla ya miradi ya maendeleo 67 ya Mkoa wa Geita. Miradi hiyo inathamani ya Tshs Bilioni 4,464,623,471/= fedha ambazo ni michango ya serikali kuu, wananchi, Halmashauri za Wilaya na Wahisani mbalimbali. |