Mheshimiwa Makamu wa Rais akimjulia hali mzazi baada ya kutembelea wodi ya wazazi na akina mama katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita. Akiwa katika hospitali hiyo aliwataka wakunga pamoja na madaktari kuhakikisha kuwa hakuna kifo chochote cha akina mama na watoto kinachotokea kwa sababu ya uzembe wa daktari au mkunga. Aidha, aliwataka akina mama kuhakikisha wanakwenda kijifungua katika hospitali kwakuwa kuna huduma nzuri kuliko majumbani na kwa wakunga wa jadi.