MATUKIO MBALIMBALI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA MKOA WA GEITA
Mgeni Rasmi wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika , Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Manzie Mangochie ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Geita akihutubia hadhara iliyojitokeza katika maadhimisho hayo amabapo aliwataka wazazi na walezi wa watoto kuhakikisha kuwa wanawapa watoto haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na Elimu na kuacha tabia ya kuwatumikisha watoto katika kazi ngumu. Aidha katika maadhimisho hayo mgeni rasmi alitoa zawadi kwa wanafunzi watatu waliofanya vizuri katika mtihani wa kumaliza kidato cha nne mwaka 2013.