Mkoa wa Geita umepiga marufuku
kwa makampuni ya uchambuzi na ununuzi wa pamba kuacha tabia ya kukopa pamba
kutoka kwa wakulima.
Akizungumza katika kikao cha sita
cha wadau wa sekta ndogo ya pamba Mkoa wa Geita Mwenyekiti wa kikao hicho
Magalula Saidi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita alisema kuwa ‘’ ni marufuku
kwa kampuni yeyote ile inayonunua pamba katika Mkoa wa Geita kukopa pamba
kutoka kwa wakulima kwani kufanya hivyo ni kumdumaza mkulima na kumcheleweshea
maendeleo yake ya kila siku’’.
Mkoa wa Geita unatekeleza kilimo
cha pamba cha mkataba ambapo wakulima wanakopeshwa pembejeo bora kutoka kwa makampuni ili wazalishe kwa
wingi na wanufaike na kilimo hicho.
Kikao cha sita cha wadau wa sekta
ndogo ya pamba Mkoa wa Geita kilifanyika kwa lengo la kufanya tathimini ya
kilimo hicho na changamoto zake kwa msimu unaokwisha 2013/2014 na pia kujadili
namna kilimo hicho kitakavyoendeshwa kwa
msimu ujao.Hatahivyo wakulima wengi wa Mkoa wa Geita wanaonyesha kukubaliana na
kilimo hicho ambacho inasemekana kina tija kwao.