Mgeni rasmi wa ufunguzi wa sherehe za maonyesho ya siku ya wakulima (nanenane) kanda ya ziwa Mhe. Magalula Saidi Magalula Mkuu wa Mkoa wa Geita watatu kutoka kushoto akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa sherehe hizo.Wakwanza kushoto ni ndugu Severine Kahitwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, wapili kutoka kushoto ni Mhe. Evarist Ndikilo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Katika ufunguzi huo Mgeni rasmi alitoa wito kwa wananchi wote wa kanda ya ziwa kutembelea mabanda yote ili wakajifunze teknolojia mbalimbali zinazotumika katika uzalishaji. Aidha, aliwataka wakulima wazalishe kwa tija kwa kutumia kanuni na mbinu bora za kilimo na mifugo kwa lengo la kuhakikisha kuwa mazao yanayozalishwa ni bora na yanayokidhi mahitaji ya soko kwani biashara ya sasa ni ya ushindani.