Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi Magalula akisalimiana na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachael Kassanda baada ya Mwenge wa Uhuru kuwasili Mkoani Geita tarehe 25/09/2014 ukitokea Mkoa wa Mwanza.Ukiwa katika Mkoa wa Geita Mwenge wa Uhuru ulipitia jumla ya miradi 75 yenye thamani ya Tshs 8,087730919.5/=. Miradi hiyo ilijumuisha sekta mbalimbali kama maji, mifugo, kilimo, ujenzi, utawala, elimu, afya, ushirika, mazingira na biashara.Ukiwa katika Mkoa huu Mwenge ulikimbizwa umbali wa Km 701.01 kabla ya kukabidhiwa katika Mkoa wa Shinyanga tarehe 01/10/2014. |