MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Thursday, 15 January 2015

Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa akifungua Mkutano wa wadau wa Sekta Ndogo ya Pamba Mkoa wa Geita ambapo aliwataka wachambuzi wa Pamba kupitia umoja wao (UMWAPA) kutekeleza Kilimo cha Pamba Cha Mkataba kwa kusambaza Mbegu za Pamba pamoja na Viuadudu (dawa) ili kuepusha hasara kwa wakulima ambao wanalima Pamba lakini Pamba hiyo inashambuliwa na wadudu kwasababu ya makampuni ya ununuzi wa Pamba ambayo wanaingia nayo Mkataba yanachelewa kufikisha viuadudu hivyo kwa wakati. Aidha, katika Mkutano huo Mkuu wa Mkoa aliwataka wachambuzi hao kuhakikisha kuwa wanasambaza mbegu kwa ujazo  tofauti wa kuanzia kilo 50, 25 na 10 ili kuondoa malalamiko ya wakulima kupunjwa na mawakala wasio waaminifu. Mkoa wa Geita unatekeleza Kilimo cha Pamba cha Mkataba kwa kuwaunganisha wakulima wa zao hilo pamoja na Makampuni ya uchambuzi ambayo yanawakopesha pembejeo wakulima na baadae kurejesha gharama hizo kwa kuuza pamba kwa makampuni waliyoingia nayo mkataba. Kilimo hicho kwasasa katika Mkoa kinaanza kuonyesha mafanikio baada ya wakulima wengi kuingia katika utaratibu huo hivyo Mkoa unatarajia ongezeko la uzalishaji wa zao la pamba.