Katibu wa Chama cha wafanyakazi (TUGHE) Mkoa wa Geita Bi. Ethel Kahuluda akizungumza na wajumbe wa baraza ambapo aliwaeleza namna wafanyakazi wanavyotakiwa kuwa wakati wa kutimiza majukumu yao ya kila siku na pia pale wanapozungumza na viongozi au waajiri wao. Alisema kuwa wafanyakazi wana kero nyingi zinazowakabili lakini ni vyema wakawa wavumilivu na watulivu wakati wa kudai haki zao za msingi napia wahakikishe kuwa pamoja na kudai haki hizo pia watimize wajibu wao ipasavyo wakati wa kuhudumia wananchi.