MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Friday, 10 July 2015

FAHAMU YALIYOJILI MKOANI GEITA WAKATI WA UFUNGUZI WA TAMASHA LA LIVE YOUR GOALS NA MAFUNZO YA GRASSROOTS YALIYOANDALIWA NA TFF PAMOJA NA FIFA

Mheshimiwa Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa Geita akizumgumza na wadau wa mpira wa miguu wa wanawake pamoja na wananchi (hawapo katika picha) wakati wa ufunguzi wa Tamasha la  LIVE YOUR GOALS na Mafunzo ya Grassroots kwa walimu wa shule za msingi yaliyofanyika katika Mkoa wa Geita kwa lengo la kuhamasisha watoto wa kike kushiriki katika mpira wa miguu.  Katika Tamasha hilo mheshimiwa Fatma Mwassa alitoa rai kwa wazazi wote kuona umuhimu wa kuwaruhusu watoto wao wa kike kushiriki katika michezo hususani mpira wa miguu kwakua michezo ni fursa na inasaidia kujenga mwili na akili na pia kuna fursa nyingi za kimaendeleo.  Pia aliwapongeza walimu wote waliopata mafunzo hayo na kuwataka kutumia ujuzi huo kwa faida ya mkoa wa Geita na Taifa kwa ujumla. "Nafahamu kuwa walimu kutoka wilaya zote na Halmashauri sita za Mkoa wa Geita wameshiriki ipasavyo katika mafunzo haya, ni imani yangu taaluma hii itafika katika shule zote za Mkoa wa Geita ili kufanya program hii kuwa endelevu''.  Hata hivyo aliwapongeza FIFA na TFF kwa kuuchagua Mkoa wa Geita kuwa wakwanza katika kutekeleza program hii ambapo aliahidi kuanzisha mashindano mengine katika Mkoa yatakayojulikana kwa jina la Blatter Cup (IF YOU DO FIFA DOES)