Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi akizungumza na wanafunzi wa shule ya Sekondari Busolwa wakati wa ziara ya kikazi wilaya ya Nyang'hwale hivi karibuni. Ziara hiyo ilikuwa na lengo la kukagua utengenezaji wa madawati katika shule za msingi na pia kukagua upelekaji wa wanafunzi waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za sekondari wilayani humo mwaka 2014.