MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Wednesday 16 April 2014

MKOA WA GEITA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU

Serikali Mkoa wa Geita imejidhatiti kuboresha hali ya Elimu katika Mkoa kwa kuboresha miundombinu ya shule na usimamizi makini.

Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Magalula Saidi wakati akiwahutubia wadau wa Elimu Mkoa wa Geita katika kikao kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya wasichana ya Nyankumbu Mkoani hapa.

"Miundombinu ya shule katika shule za Msingi na Sekondari siyo ya kuridhisha hasa upungufu wa madawati katika shule za msingi Wito wangu kwenu ninyi wadau ongezeni jitihada ya kuwahamasisha wananchi kutengeneza madawati ili kupunguza tatizo hili katika shule zetu.Halmashauri zikumbuke kutenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hasa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na matundu ya vyoo kwa ajili ya shule za msingi na sekondari" alisema Mkuu wa Mkoa.

Wadau wa elimu Mkoa wa Geita walikutana pamoja ili waone namna ya kuweka mikakati itakayosaidia kuimarisha hali ya elimu katika Mkoa.

Mkoa wa Geita umepiga hatua katika uandikishaji wa wanafunzi wa awali ambapo kwa mwaka 2014 asilimia 79.4% ya wanafunzi wameandikishwa, kwa darasa la saba ni 91%.Mwenendo wa kuripoti shuleni kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza ni asilimia 84%.Wito umetolewa kwa wadau wote kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaripoti shule haraka iwezekanavyo, na wazazi wote ambao hawajapeleka watoto wao shule wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

Katika kuhakikisha kuwa tatizo la mdondoko mkubwa na utoro unaozikabili shule za mkoa wa Geita unakomeshwa wadau wametakiwa kuhakikisha watoto walioripoti shuleni wanahudhuria kila siku bila kukosa.
Magesa Jumapili: