Mkuu wa Mkoa wa GeitaMhe.Magalula Saidi akikabidhiwa madawati na Meneja wa NMB kanda ya ziwa ndg. John Chilongola wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mji wa Geita. |
Benki ya NMB Tawi la Geita Mkoani hapa
imechangia vifaa vyenye thamani ya Tsh. 25 million katika Sekta ya Afya na
Elimu. Mchango huo unatokana na ahadi
iliyotolewa na Benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa Mkoa wa Geita mnamo
tarehe 08/11/2013 alisema Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Bw. Severine Kahitwa
alipokuwa akifungu hafla hiyo fupi.
Akizungumza katika makabidhiano hayo
Meneja wa NMB Kanda ya Ziwa Ndugu John Chilongola alisema kuwa ni utaratibu wa
Benki hiyo kutoa msaada katika jamii inayozungukwa na Benki hiyo ili kutatua
changamoto zinazokabili jamii katika sekta ya elimu na afya.
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa vina
thamani ya Tshs. 25million ambapo ni madawati 100 yenye thamani ya Tshs.
10mill, mashuka 500, vitanda viwili vya kujifungulia na vitanda 10 vya wagonjwa
na magodoro yake.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa
hivyo Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Geita Magalula Said Magalula aliwapongeza sana
viongozi wa Banki hiyo kwa kuona umuhimu wa kuusaidia Mkoa wa Geita katika
sekta za Afya na Elimu kwani Mkoa una upungufu mkubwa sana wa madawati na vifaa
vya Afya.
Aidha, alitoa wito kwa wananchi na
wadau wengine wenye moyo kuendelea kutoa michango hiyo ya hali na mali ili
kuweza kusaidia katika sekta mbalimbali ndani ya Mkoa na aliahidi kuwa vifaa
hivyo vitatunzwa na kufikishwa katika maeneo husika.
Aliwaomba viongozi wa dini
waliohudhuria hafla hiyo kutangaza matatizo yanazozikabili sekta mbalimali ili
wananchi wahamasike kuchangia huduma hizi
muhimu.
Katibu Tawala Mkoa wa Geita alitoa
maelekezo dhidi ya mgao wa vifaa hivyo katika Halmashari zote ambapo alieleza
kuwa mashuka 100 yanakwenda kituo cha Afya Msumbwe Wiaya ya Mbogwe, mashua 100
yanakwenda kituo cha Afya Bwerwa Wilaya ya Mbogwe, mashuka 100 yanakwenda kituo
cha Afya Kharumwah Wilaya ya Nyang’hwale, kituo cha Afya Kachwamba Wilayani
Chato mashuka 50, kituo cha Afya Bulega mashuka 50 Wilaya ya Bukombe, Chikobe
mashuka 50 na Kashishi mashuka 50 Wilaya ya Geita.
Madawati 100 yanakwenda katika shule ya
msingi Nyanza iliyopo Kata ya Kalangalala ili kumaliza tatizo la madawati
katika shule hiyo. Wakati vitanda viwili vya kujifungulia vinakwenda katika
vituo vya Kharumwah na Iboya.
Msaada huu umekuja katika muda muafaka
wakati Mkoa wa Geita ukiwa katika mkakati mkubwa wa kuboresha sekta za elimu na
afya.
Na: Magesa Jumapili.