MAWASILIANO YA BLOG

KWA MAONI NA USHAURI WASILIANA NA OFISI YA HABARI NA MAWASILIANO KWA SIMU NAMBA 0764 143 977 AU E-MAIL: habarigeita@gmail.com

Friday, 11 November 2016

PSPF MKOA WA GEITA WACHANGIA MADAWATI 100 YENYE THAMANI YA TSHS 7.5 MILIONI MKOANI GEITA

Edward Temu Kaimu Mkurugenzi wa PSPF Mkoa wa Geita  akikabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi 7,500,000/= kwa Mheshimiwa Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Halmashauri ya Mji Geita. Mkuu wa Mkoa amewashukuru PSPF kwa mchango wao huo wenye manufaa katika Sekta ya Elimu Mkoani Geita na ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na wadau wote wa maendeleo kuendelea kuchangia madawati ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wote katika Mkoa wa Geita wanakaa kwenye madawati wakati wa masomo yao katika shule zote za Msingi na Sekondari. Madawati yote yaliyopokelewa yamepelekwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ili kupunguza uhaba huo katika Halmashauri hiyo. 

Mwenyekiti wa kamati ya Madawati Mkoa wa Geita Atanazy Enyasi akizungumza na ndugu  Elias Kayandabila Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe baada ya kumkabidhi madawati 100 yenye thamani ya shilingi 7.5 Milioni ikiwa ni mchango wa shirika la PSPF Mkoa wa Geita.

Viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoa wa Geita wakiwa wamekaa pamoja na wanafunzi kwenye madawati 100 yaliyotolewa na PSPF Mkoa wa Geita.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Selestine Gesimba akisisitiza jambo wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa madawati 100 iliyoandaliwa na PSPF Geita. Ndugu Gesimba amewashukuru wadau wote wanaondelea kutekeleza ahadi yao walio ahidi wakati wa harambee ili kukamilisha na kumaliza tatizo la madawati katika Mkoa wa Geita.

Mheshimiwa Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akikabidhi madawati 100 kwa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Madawati Mkoa wa Geita ndugu Atanazy Enyasi na Ernest Nyororo. Madawati hayo kutoka PSPF yamekabidhiwa kwa Halmashauri ya Mbogwe.


Mzee Atanazy Enyasi Mwenyekiti wa kamati ya madawati Mkoa wa Geita akizungumza  na kuwaomba wananchi na wadau wengine wa maendeleo kujitokeza na kuchangia madawati wakati wa hafla fupi ya Mkoa wa Geita kupokea madawati 100 kutoka katika mfuko wa hifadhi ya Jamii wa PSPF Geita.

Wanafunzi wakiwa wamekalia sehemu ya madawati iliyochangwa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa PSPF

Mheshimiwa Meja Jenerali (Mst) Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Geita walioshiriki katika hafla fupi ya kukabidhi madawati  100 iliyoandaliwa na PSPF Geita katika viwanja vya Halmashauri ya Mji Geita.

Monday, 15 August 2016

WAKAZI WA GEITA KUPATIWA MAGWANGALA (MIAMBA TAKA) KUTOKA MGODI WA GGM BAADA YA SERIKALI KUTENGA MAENEO YA SAMINA ''B'', LWENGE NYAMIKOMA NA KASOTA ''B''


Mheshimiwa Meja Jenerali (MST) Ezekiel E Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akisoma taarifa kwa Waziri wa Nishati na Madini kuhusu maeneo yaliyotengwa na Mkoa kwa ajili ya Shughuli za Uchenjuaji wa Miamba taka itakayotolewa katika Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM). Maeneo yaliyotengwa yamezingatia vigezo vya utunzaji wa mazingira pia afya za wananchi.  Maeneo hayo ni pamoja na eneo la Lwenge Nyamikoma, Kasota "B'' (Halmashauri ya Wilaya Geita) na eneo la Samina ''B'' lililopo Halmashauri ya Mji Geita. Wananchi wametakiwa kuunda vikundi na kuvisajili ili kupatiwa miamba hiyo kwa kuwa haitatolewa kwa mtu mmoja mmoja. Zoezi hili ni utekelezaji wa Agizo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilolitoa tarehe 31/07/2016 wakati wa ziara yake Mkoani hapa, pia ni juhudi za Serikali kuwawezesha wananchi ili wajipatie kipato cha kuendesha maisha ya kila siku na kupata maendeleo.


Mheshimiwa Sospeter Mhongo Waziri wa Nishati na Madini akizungumza na Viongozi mbalimbali na Wadau wa Mazingira wa Mkoa wa Geita wakati wakati wakikagua maeneo ya kumwaga miamba taka kutoka Mgodi wa GGM. Kulia kwa Waziri ni Selestine Gesimba Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita na Kushoto ni Ali Kidwaka Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Geita.

Sunday, 14 August 2016

Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Viongozi na wadau wa Mazingita Mkoa wa Geita wakikagua maeneo ambayo miamba taka (Magwangala) yatamwagwa kwa ajili ya Uchenjuaji wa Dhahabu kwa vikundi  vitakavyoundwa.

Sunday, 24 April 2016

MKUU WA MKOA WA GEITA MEJA JENERALI EZEKIEL KYUNGA ATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA NYUMBA 18 ZA WATUMISHI, HOSPITALI TEULE YA MKOA WA GEITA NA SOKO LA WAKULIMA NYANKUMBU HALMASHAURI YA MJI GEITA


Mheshimiwa Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa Geita akizungumza na mjasiliamali wa kuuza viazi vitamu Bi. Aneth Mabula katika Soko la wakulima Nyankumbu Halmashauri ya Mji Geita alipotembelea soko hilo hivi karibuni. Akiwa sokoni hapo Mkuu wa Mkoa alisisitiza suala la usafi katika maeneo yote ya Soko. Aidha aliwaeleza wafanya biashara kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha ina boresha soko hili ili wananchi wafanye biashara katika mazingira mazuri na salama kwa afya za wateja wao.


Katika ziara hiyo Mkuu wa pia alipata fursa ya kutembelea Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita kwa lengo la kuona namna huduma kwa wananchi zinavyotolewa katika Hospitali hiyo. Aidha, alipongeza juhudi za kampuni ya Mgodi wa Geita (GGML) Katika kusaidia kuboresha huduma za afya kwa kununua vifaa vya kisasa.  Hata hivyo aliwataka watumishi wa Idara hiyo kufanya kazi kwa weledi ili kutatua matatizo ya wananchi wanaofika katika Hospitali hiyo kupata Huduma.

Moja ya Nyumba za watumishi wa Halmashauri ya Mji Geita zilizotembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita katika eneo la Bombambili.Nyumba hizi zimejengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Mkuu wa Mkoa  wa Geita akiongozana na viongozi  wa Wilaya ya Geita kukagua mradi wa nyumba 18 za watumishi  zilizonunuliwa na Halmashauri ya Mji Geita kutoka Shirirkr la nyumba la taifa (NHC) ili kusaidia kuboresha makazi ya watumishi katika Halmashauri hiyo.(Wakwanza kulia ni Manzie Mangochie Mkuu wa Wilaya ya Geita).


Baadhi ya nyumba zilizotembelewa na kukaguliwa zinavyoonekana.Nyumba hizi zina uwezo wa kuhudumia familia mbili kwa wakati mmoja.

Watumishi pamoja na viongozi wa Serikali Mkoani Geita wakifuatilia kwa karibu maelekezo ya  Mkuu wa Mkoa wa Geita alipofanya ziara katika Halmashauri ya Mji Geita.

Mheshimiwa Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita akizungumza na vyombo vya Habari pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali Mkoani Geita kueleza madhumuni ya Ziara yake katika Halmashauri ya Mji Geita.

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mji Geita Ndugu Max Kamaoni akisoma taarifa ya miradi ya maendeleo ambayo imetembelewa na Mheshimiwa  Meja Jenerali (Mstaafu) Ezekiel Kyunga Mkuu wa Mkoa wa Geita (hayupo kwenye picha) wakati wa ziara yake ya kikazi katika Halmashauri hiyo tarehe 23/04/2016.(PICHA  OFISI YA RC - GEITA).

Monday, 21 March 2016

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AMWAPISHA JENERALI EZEKIEL ELIAS KYUNGA KUWA MKUU MPYA WA MKOA WA GEITA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuri akimwapisha Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuwa Mkuu  mpya wa Mkoa wa Geita wakati wa hafla ya kuwaapisha wakuu wa Mikoa Ikulu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita mheshimiwa Ezekiel Eliasi Kyunga akimkabidhi hati ya kiapo Mheshimiwa Rais  baada ya kuapishwa.

Tuesday, 2 February 2016

MHESHIMIWA SAMIA SULUHU MAKAMU WA RAIS AZINDUA WODI YA WAGONJWA WA DHARULA, MRADI WA MAJI, KIKUNDI CHA USHONAJI CHA AKINA MAMA NA VIJANA , MITAMBO YA UJENZI WA BARABARA MKOANI GEITA.

Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akikabidhi Mashine ya Echo Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Joseph Kisala alipotembelea Hospitali hiyo na kuzindua wodi ya wagonjwa dharula na wodi ya watoto. Mashine hiyo ni moja kati ya vifaa vya kisasa ambavyo vimewekwa katika Hospitali hiyo na serikali kwa lengo la kuhakikisha kwamba wananchi wanapata huduma bora za Afya na kwa wakati. Aidha katika ziara hiyo Makamu wa Rais alizindua mitambo ya kuchuja maji Nyankanga na kituo cha maji Nyankumbu , Mradi huo utasaidia zaidi ya watu 4000 kupata maji safi na salama. Pia, alitembelea mradi wa ushonaji wa akina mama na vijana wa kikundi cha Nyakatoma ambao unalenga kuwaendeleza vijana na wanawake ili kujipatia maendeleo. Vilevile alizindua mitambo ya ujenzi wa barabara yenye thamani ya tshs 2.1 bilioni fedha ambazo zilitokana na mapato ya ndani ya Halmashauri ya Mji Geita. Mitambo hiyo itasaidia kuboresha miundombinu ya barabara na kusidia kupunguza gharama katika mitambo ya kukodi na kuongeza kipato kwa Halmashauri hiyo.


Kikundi cha akina mama na vijana cha ushonaji Katoma kilichotembelewa na Makamu wa Rais.

Wananchi wakimsikiliza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais akiweka jiwe la msingi la uzinduzi wa mitambo ya kuzalisha maji Nyankanga Geita Mjini ambayo itazalisha maji ya kutosha  watu zaidi ya 4000 itakapokamilika.Mradi huo unatekelezwa kati ya serikali na mgodi wa Geita Gold Mine kwa lengo la kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maji safi na salama.

Makamu wa Rais akikata utepe wakati akizindua mitambo ya kuzalisha na kuchuja maji katika eneo la Nyamkanga Mradi huu utahudumia wananchi zaidi ya 4000.

Mitambo ya ujenzi wa barabara iliyonunuliwa na Halmashauri ya Mji Geita na kuzinduliwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mji Geita Max Kamaoni akisoma taarifa ya ununuzi wa mitambo ya ujenzi wa barabara ambayo ilizinduliwa na Mheshimiwa Makamu wa Rais yenye thamani ya Shilingi 1.2 bilioni fedha ambazo ni mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo. Makamu wa Rais alipongeza jitihada zilizofanyika mpaka kupata mitambo hiyo muhimu kwa maendeleo ya Halmashauri hata, hivyo aliagiza kuwa mitambo hiyo itunzwe na itumike kwa kazi zilizokusudiwa.

Mheshimiwa Makamu wa Rais akizungumza na wananchi wa Geita awapo kwenye picha wakati wa ziara yake Mkoani hapa.

Kwaya ya Yeriko AIC Geita ikitumbuiza wakati wa ziara ya Makamu wa Rais Mkoani Geita.


Wananchi pamoja na watumishi wa idara ya Afya wa Mkoani Geita wakifuatilia kwa karibu maelekezo ya Mheshimiwa Makamu wa Rais wakati akizungumza nao hivi karibuni.

Mheshimiwa Makamu wa Rais akiongozana na viongozi mbalimbali wa kitaifa na Mkoa wa Geita wakati wa ukaguzi wa Hospitali Teule ya Mkoa. Kutoka kulia ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, kushoto ni Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita , mwingine ni Mhe. Vick Kamata (Mb).

Mkuu wa Mkoa wa Geita Fatma Mwassa akijadili jambo na Mheshimiwa Samia Suluhu Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa ziara yake Mkoa wa Geita.

Viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi wakimsikiliza Mheshimiwa Makamu wa Rais hayupo pichani wakati wa ziara yake ya siku moja Mkoani Geita.