MKOA WA GEITA WAWAFARIJI WAANGA WA MAAFA YA MVUA KUBWA HUKO MWAKATA WILAYA YA KAHAMA
Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akimkabidhi Benson Mpesya Mkuu wa Wilaya ya Kahama Gunia la mchele kuwakilisha bidhaa nyingine zilizotolewa na Mkoa wa Geita kwa wananchi wa kijiji cha Mwakata ambao walipatwa na maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa na upepo mkali na kupelekea watu zaidi ya 30 kupoteza maisha pamoja na uharibifu mkubwa wa mali za wananchi ikiwemo mifugo na makazi.Katika salamu zake Mkuu wa Mkoa alitoa rai kuwa msaada huo utumike kama ulivyokusudiwa na kuwafike walengwa.Aidha, aliwataka wananchi kuwa watulivu wakati serikali na wadau wengine wakiendelea na jitihada za kuwasaidia.Bidhaa zilizotolewa na Mkoa wa Geita ni pamoja na Mchele, Maharage, Unga n.k.Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Bw. Charles Pallangyo pamoja na wakurugenzi wote wa Halmashauri za Mkoa wa Geita.