Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini akiwakabidhi hundi ya Tshs bilioni 2.23 wenyeviti wa Halmashauri ya Geita na Halmashauri ya Geita Mjini. Fedha hiyo inatokana na kodi ya ushuru wa tozo (service levy) iliyolipwa na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Geita (GGML). Aliwataka Wenyeviti hao kuhakikisha kuwa fedha hizo zinafanya kazi za maendeleo na siyo vinginevyo ili kukuza uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Geita. Hata hivyo aliwaeleza wananchi kuwa watarajie kuona huduma bora zaidi kwenye elimu, afya, barabara, umeme na maji. Kampuni ya GGM imekuwa ikisaidia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mkoa huu kama vile ujenzi wa shule,ujenzi wa nyumba za watumishi na kituo cha afya Nyakabale, maji na kituo cha ushauri nasaha Geita. |