Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Geita akiongozana na Mhe. George Simbachawene Waziri wa Nishati na Madini wakati wa ukaguzi wa miundombinu ya maji ambayo inatarajia kusambaza maji mjini Geita. Mradi huo wa maji wa Mjini Geita unatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya uchimbaji wa madini Geita (GGML). Mradi huo unatarajiwa kukamilika mapema mei 2015.